Parish Details
Kanisa la Mt. Cecilia BUJORA
Najua umewahi kuona makanisa mengi hapa africa ambayo mara zote yamekuwa yakijifananisha na tamaduni za ulaya kutokana na historia ya kanisa ilivyo. Makanisa yote yamekuwa yakijengwa kufananishwa na jinsi makanisa ya KIZUNGU yalivyo na kuitwa majina ya huko yalipoanzia na pia kuwaonesha Yesu na mitume wake kama wazungu n.k
Sasa, kuna kanisa lipo
Bujora Mwanza. Hili ni la kipekee! Lilijengwa na mzungu lakini kini limejengwa
kwa kufuata tamaduni za kisukuma. Kuanzia jengo na vitu vilivyomo ndani na hata
sanamu ndani ni za sura za kiAfrica pamoja na Yesu mwafrica. Inapendeza sana jinsi
ambavyo jamii hii ya wasukuma ilivyofikiwa na hawa wamishionari. Hebu jionee
mwenyewe hizi picha za kanisa hilo.