• archmwanza@gmail.com
  • +255 769 523 036

Historia Fupi Ya Parokia Ya Ng'hungumalwa

Parish Details

HISTORIA FUPI YA PAROKIA TEULE YA

MT. PETRO MTUME  -  NG’HUNGUMALWA.

 

Kigango cha Ng’hungumalwa kilianzishwa mnamo mwaka 1974 kikitokea Mwamhaya ambako waamini wa Nyanhiga na Ng’hungumalwa walikuwa wanasali Mwamhaya. Katekista wa Mwamhaya kwa wakati ule alikuwa ni Yakobo Mviji. Baada ya kuanzishwa kigango cha Ng’hungumalwa, Katekista wa kwanza alikwa Bonaventura Fugongali (Marehemu).

 

Waumini walianza kusali katika eneo ambalo hapakuwa na jengo lolote, walianzia palipo na machinjio kwa sasa. Mwaka 1975 waliomba kiwanja katika serikali ya Kijiji, walipewa eneo la ekari 1.5 ambapo waliendelea kusali hadi mwaka 1988 ambapo kiwanja kilikatwa na grid ya Taifa mwaka 1989, waliomba tena eneo jingine ambalo wanalo mpaka sasa. Baada ya kupewa na serikali ya Kijiji kiasi cha ekari 33.

 

Makatekista wa kwanza ni:- Bonaventura Fugongali, Leontina Shigu, Gaspar Luhonola, Berali Mbilingi, Didas Budila, Lucas Gunanangila, Deogratias Bugode, Francis Tissian, Mariana Kundi, Clement Shilinde hadi sasa.

 

Mwaka 1996 ulitokea mgogoro katika eneo la kanisa dhidi ya Mwenyekiti wa Kijiji aliyehodhi ardhi ya Kanisa kwa mamlaka aliyokuwa nayo, kesi hiyo ilidumu miaka 3 na kumalizika mwaka 1998 ndipo Kanisa liliposhinda kesi mahakamani.

 

Shukrani kwa Deogratias Kibungi Mwenyekiti wa Kigango wakati ule (Marehemu), aliyesimamia kesi hadi haki     ikapatikana. Pia kwa Bonaventura Fugongali Katekista              wakati ule (Marehemu) aliyetoa Ushahidi mahakamani. Pia tunamshukuru Clement Shilinde katibu wa Kigango wakati ule aliyetoa Ushahidi Mahakamani hadi haki ikapatikana. Pia Mzee Sabini Ngeleja alikuwa mshauri katika kesi hiyo.

 

Kigango cha Ng’hungumalwa kilikuwa sehemu ya Parokia ya Mt. Anna Mwabagole ikiongozwa na Padre Karoli Zimameni (Paroko) na Padre Ferdinand Baremare (Paroko msaidizi ) wakitokea katika shirika la White Fathers.

 

Katika kukua na kuimarika kiimani, kigango cha Ng’hungumalwa kilirasimishwa na kupandishwa hadhi na kuwa Parokia Teule mnamo tarehe 04/08/2016 na                      Mhashamu Askofu Mkuu Juda Thadeus Ruwa’ichi aliyekuwa askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza.

 

B.  MAPADRE WALIOWAHI KUHUDUMU PAROKIA TEULE HII YA NG’HUNGUMALWA

 

Katika historia, Kanisa kwanza linawashukuru mapadre wote waliowahi kutoa huduma za kiroho na kuchangia kukuza na kuimarisha imani kwa waamini hapa                    Ng’hungumalwa; Padre Karoli Zimameni, Pd. Ferdinand Baremare, Pd. Francis Bahebe, Pd. John Buluma, Pd. Justine Mabula, Pd. Bruno Mahenda, Pd. Pius bilulu, Pd. Mathayo Bujiku, Pd. Claud Mpuya, Pd. Robert Kitambo, Pd. Francis Mtema, Pd. Maximilian Buluma, Pd. Andrea Msonge, Pd. Zacharia Makoye, Pd. Casmir Bulugu, Pd. Christopher Baluhya, Pd. Mikael (SMA), Pd. Thomas (SMA), Pd. John Krikoin (SMA), Pd. Misheli (SMA), Pd. Anthon Lachaga (SMA), Pd. Deogratias Malekanya.

 

Hali kadhalika tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa mapadri wafuatao kwa kuendelea kutoa huduma na kushirikiana na Parokia kwa ujumla, kwani wamekuwa chachu ya kuimarika kiroho na maendeleo ya kanisa kwa ujumla yaani:- Pd. Costantine Sendama (Paroko Nyabulogoya), Pd. Theophil Kumalija (Parokia ya Sahwa), Pd. Pd. John Nkwabi ( Paroko Tarazo), Pd. George Nzungu (Paroko Nyamhongolo), Pd. John Kasembo (Paroko Kitumba), Pd.Gerald Kabomo (Kawekamo na Ofisi ya Askofu Mkuu), Pd. William Ndonhe (Nyegezi Seminari).

 

Hali kadhalika, tunamshukuru padre Raso Litaka wa Jimbo la Mahenge anayefanya utume katika Seminari Kuu ya Mt. Paul Kipalapala Jimbo Kuu la Tabora, kwa majitoleo na muda wake kwa ajili ya kutoa huduma katika parokia yetu inayozinduliwa leo.

 

Pia tunamshukuru padre Charles Masaga (Dokta Maua) toka parokia ya Nyabulogoya kwa kuwa bega kwa bega na waumini hadi leo hii tumefikia kuzinduliwa. Amehudumu hapa na kushauri mambo mengi.

 

Wote hawa wamekuwa msaada mkubwa sana katika kutoa huduma za kiroho katika parokia hii Teule; Ahsanteni sana Mungu awape afya njema.

 

Pia kwa namna ya pekee tunamshukuru sana Baba Paroko wetu Pd. Fabian Mhoja (Shigulu shabuki) anayehudumia mpaka sasa kwa kutuongoza vyema na kutoa huduma za kiroho katika maeneo yote ya vigango vyetu. Baba Paroko wetu amekuwa mtumishi na chachu ya maendeleo ya Parokia Teule hii kwa kuhamasisha na kufundisha imani thabiti ya kanisa na uchungaji mwema hasa kwetu sisi. Pia tunamshukuru kwa uhamasishaji wa maendeleo ya kanisa hasa kwa kuhamasisha ujenzi wa nyumba ya mapadre vigango na kanisa kwa ujumla; tunasema asante sana Mungu akujalie afya njema na utume mzuri uendelee kutuhudumia.

 

 

C. VIONGOZI HALMASHAURI WALEI

 

Tunawashukuru sana viongozi waanzilishi wa kigango waliotumika kuasisi na waanzilishi kama ifuatavyo:-

 

Mzee Aloyce Petro (Marehemu), Mzee Deogratias Kibungi (Marehemu), Mzee Clement Kalemani (Marehemu), Mzee Stephen Yamala, Daniel, Magdalena Joseph (Marehemu), Marietha Petro (Marehemu), Anastazia na Temela. Hawa walifanya utume wao vizuri na mwenyezi Mungu awarehemu wote waliotangulia mbele za haki na wale waliopo hai Mungu awazidishie kwa kutumika na utume wenu Baraka zake zikae nanyi na familia zenu. 

 

VIONGOZI WALIOPO KWA SASA MPAKA LEO

 

Viongozi hawa tunawaombea waendelee na utume wao kwa kumtanguliza Mungu  zaidi maana wamechaguliwa na Mungu na tunawashukuru kwa kuendelea kutumikia kanisa hadi leo tunapozinduliwa kuwa Parokia rasmi. Shukrani nyingi kwa hawa wafuatao; Deogratias Masanja (Mwenyekiti), Deogratias Fabian (M/Mwenyekiti), Zakayo Togoi (Katibu), Leonard Justine (M/Katibu) Thelezia Andrea (Mhasibu) na Richard B. Stephen (Katibu Mtendaji).

 

MAKATEKISTA

Walezi wetu wa kiroho makatekista wanaohudumu katika parokia Teule hii mpaka sasa tunao Makatekista wafuatao:- Clement Shilinde (Mwenyekiti), Stephen Henerco (M/Mwenyekiti), F. Bunane (Katibu), Mariana Shilinde

 

(Mhasibu) Gerald Gasembe (Mratibu), George, Yulitha Shilangi, Francis Tisian, Justine Philipo, Raphael Luhunga, Felister John, Razalo Masele, Maria Makaji, Costantine Busongo, Paulo Lugolola, Sylivester na Aloyse John (Katibu Msaidizi).

 

MAKATEKISTA WAANZILISHI

Bonaventura Fugongali (Marehemu), Leonstina Shigu (Marehemu), Gaspary Luhonola (Marehemu), Didas Bundila (Marehemu).

 

MAKATEKISTA WASTAAFU

Paschal, Deogratias, Elias Masheku.

 

JUMUIYA

 

Wakati Kigango kinaanzishwa kilikuwa na Jumuiya ndogondogo za Kikristu tatu (3) tu ambazo ni Moyo Mtakatifu wa Yesu, Rozali Takatifu na Utatu Mtakatifu. Pia kigango kilianza na familia za Kikristu 52 tu na sasa hivi tunazinduliwa tukiwa na familia za Kikristu 1200 na Jumuiya za Kikristu 75. Tunashukuru Mungu kwa Injili                 kutufikia na kuamsha Imani na Mshikamano katika kumtangaza Kristo kama ilivyo Kauli mbiu yetu.

 

SHUKRANI

Tunakushukuru sana Mhashamu Askofu Mkuu Renatus Nkwande kwa kuridhia leo hii katika historia ya kanisa letu kuipandisha hadhi na kuzinduliwa kuwa Parokia kamili. Leo ni siku pekee sana kwa wanaparokia hii, maana ni safari kubwa na ndefu mpaka kufika leo na kusimikwa Parokia. Tunasema tena asante sana na Mungu akupe afya njema katika utume wako wa kila siku katika Jimbo letu.

 

Tunamshukuru kwa namna ya pekee Hayati Askofu Mkuu Anthony Petrus Mayala kwa kutuhimiza kununua maeneo makubwa kwa ajili ya makanisa.

 

Tunatoa shukrani za pekee kwa Mikael Majige kwa kununua eneo la Kanisa ambalo tunalitumia, yeye aliamua kutoa fidia kwa watu ambao walikuwa wanalitumia eneo hili. Yeye hakutaka kuwepo na mgogoro mwingine. Mwaka 1999, tulianzisha ujenzi wa kanisa, marehemu Mikael Majige alijitolea kujenga kanisa kwa majitoleo mengi sana vikiwemo saruji, fedha za kulipa mafundi pamoja na usafiri.

 

Tunamshukuru tena marehemu Mikael Majige, aliyethubutu kufanya majitoleo ya hali na mali kwa kanisa letu, kwa kununua ardhi ya Ekari 32 na kuitoa kwa kanisa hili. Pamoja na fedha za kuanzisha ujenzi wa kanisa tunaloliona leo. Kwa namna ya pekee alifanya tendo la pekee sana, Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani - Amina.

 

Shukrani nyingi zimwendee Padri Casmir Bulugu aliyeanzisha Msingi wa Kanisa tunaloliona leo. Pia alianzisha jingo la chekechea, tunasema ahsante sana. Tunatoa shukrani za dhati kwa WATAWA nyumba ya Mwahoba (Shirika la mabradha wa Moyo Mtakatifu wa Yesu) likiongozwa na kaimu Br. Simeon Sahani.

 

MWISHO

Tunawashukuru kwa moyo wa dhati walezi wetu Parokia ya Mt. Anna Mwabagole, wamekuwa wazazi bora na hakika wametulea katika malezi mema mpaka leo tunazinduliwa na kuwa Parokia rasmi, hii yote ni kwa malezi mazuri                               waliyotupatia ya upendo, uvumilivu na majitoleo katika misingi ya kiimani. Wametusaidia katika mengi, tunasema asanteni sana familia yote ya Parokia ya Mwabagole.

 

Parish Images

Parish Videos