MASISTA WABENEDIKTINI

Nyumba ya Masista wa Shirika la Wabenedictine wa Ndada Kawekamo Mwanza ilianzishwa baada ya ziara ya Papa Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 4 Septemba 1990, na Askofu Anthony Mayala. Ni tawi kutoka kwa Sisters wa Benedictine wa Afrika wa Mama Yetu Msaidizi wa Wakristo Ndanda Mtwara – Tanzania chini ya uongozi wa Mama Mkuu M. Auxilia Hokororo OSB. Hafla ya kwanza ya kitaaluma ilifanyika tarehe 20 Februari 1998 na jumla ya Sisters watatu, ikifuatiwa na nadhiri za milele mnamo mwaka 2007 na Sisters hao hao. Mwaliko wetu ni kumwakilisha Kristo kwa wanadamu wote kupitia uinjilisti, kuwahudumia wagonjwa na makundi yaliyo nyuma, kufundisha shule za ngazi mbalimbali, na kujenga uwezo wa wanawake katika maeneo ya vijijini. Hivi sasa, jamii ina jumla ya wagombea 12, postulants 12, novice 14, Sisters waliofanya nadhiri za muda 47 na Sisters 45 waliofanya nadhiri za milele.



MOYO MTAKATIFU WA YESU

         Shirika la Mabradha wa Moyo Mtakatifu wa yesu lilianzishwa mnamo 18.6. 1953,  na hayati askofu JOSEPH BLOMJUS Askofu wa kwanza wa mwanza,Makao yake yakiwa ni nyegezi, Shirika lilifanikiwa kupata miito ya kutosha vijana walijiunga na shirika hili  kwa nia ya kuwa watawa mabradha.Malezi yaliendelea kwa vijana  kwa hatua mbalimbali za maisha ya kiroho kutoka kwa mapadre  wamissionary. Ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya kozi mbalimbali za ufundi,ualimu na ujasiliamali .Mabradha walihitajika sana pia kwa  shughuli za ujenzi wa makanisa,shule,zahanati na makazi ya parokia, baadhi tayari walikuwa  wakitekeleza kazi hizo katika  maeneo ya  Buhingo, Sumve na Nyegezi .Baadae walifanya kazi kome na nyantakubwa .Mnamo 18.12.1965 Papa Paulo vi  alimmteua Padre  Renatus Butibubage kuwa askofu  wa mwanza.Katika kipndi cha uongozi wake, Hayati Askofu Renatus Butibubage, Mabradha  walionja hali ambayo  ilipelekea  kukosa mwelekeo mzuri wa wito wao .Lakini pamoja na  hayo matarajio ya  mwanzo hayakufanikiwa  kwani mabradha Waliokuwa wamekaribia kufunga nadhiri za daima Askofu Butibubage aliwazuia  kurudia  nadhiri zao  na kufunga kuweka nadhiri za daima hali iliyopelekea shirika kupolomoka kwani wengi wao waliondoka wakabaki wachache.Mwaka 1970  walibakia mabradha  watatu nao walikaa nyegezi  na shirika likawa limesimama. Mnamo mwaka 1989 Hayati Askofu Mkuu Antony Mayala alipochaguliwa kuwa Askofu wa Mwanza alifanya mpango wa kulihuisha upya  tena shirika hili la Mabradha wa Moyo mtakatifu wa Yesu  likiwa na mabradha wawili ambao walikuwa wamebakia.Hayati  Askofu Mkuu mayala   aliomba  mabradha wa shirika la  Banakaroli  kutoka jimbo la masaka nchini Uganda  kuja kusaidia malezi kwa shirika hili , Mpango huo ulilete mawazo chanya yaliyoweza kuzaa matunda baada ya mkuu wa shirika hilo kukubali ombi la  askofu mayala   na kuja kuanza kutekaleza kazi hiyo mara.  Banakaroli walianza kulea vijana wale walioingia kwenye malezi ya kuwa mabradha, na june  1993 wanovis waliweka nadhiri za kwanza   na shirika likaendelea    na  wanashirika walipokuwa wengi  Banakaroli walirudi shirikani kwao na wanashirika wazarendo wakashika hatamu.

     Shirika la moyo mtakatifu mpaka sasa linajumla ya mabradha 16, baadhi yao wanafanya utume maparokiani, nyumba ya askofu, taasisi na wengine wako shule na vyuoni.  Shirika hili bado liko na  mahangaiko kwani halijajiimalisha  kusimama vizuri katika Nyanja zote kwa ujumla.Shirika la Moyo Mtakatifu wa yesu  Nyumba yake mama iko MWAHOBA,Ndani ya parokia ya Nh'ungumalwa Jimbo la Mwanza.

      Utume wa shirika

                                    Kueneza injili katika jimbo kuu la Mwanza kwa kufanya huduma za kichungaji parokiani na kupokea utumishi mbalimbali katika taasisi za jimbo kuu la Mwanza kadri wakubwa wa shirika wanavyoona inafaa. Pia ukarimu wa kizalendo.