Shirika la Mabradha wa Moyo Mtakatifu wa yesu lilianzishwa mnamo 18.6. 1953, na hayati askofu JOSEPH BLOMJUS Askofu wa kwanza wa mwanza,Makao yake yakiwa ni nyegezi, Shirika lilifanikiwa kupata miito ya kutosha vijana walijiunga na shirika hili kwa nia ya kuwa watawa mabradha.Malezi yaliendelea kwa vijana kwa hatua mbalimbali za maisha ya kiroho kutoka kwa mapadre wamissionary. Ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya kozi mbalimbali za ufundi,ualimu na ujasiliamali .Mabradha walihitajika sana pia kwa shughuli za ujenzi wa makanisa,shule,zahanati na makazi ya parokia, baadhi tayari walikuwa wakitekeleza kazi hizo katika maeneo ya Buhingo, Sumve na Nyegezi .Baadae walifanya kazi kome na nyantakubwa .Mnamo 18.12.1965 Papa Paulo vi alimmteua Padre Renatus Butibubage kuwa askofu wa mwanza.Katika kipndi cha uongozi wake, Hayati Askofu Renatus Butibubage, Mabradha walionja hali ambayo ilipelekea kukosa mwelekeo mzuri wa wito wao .Lakini pamoja na hayo matarajio ya mwanzo hayakufanikiwa kwani mabradha Waliokuwa wamekaribia kufunga nadhiri za daima Askofu Butibubage aliwazuia kurudia nadhiri zao na kufunga kuweka nadhiri za daima hali iliyopelekea shirika kupolomoka kwani wengi wao waliondoka wakabaki wachache.Mwaka 1970 walibakia mabradha watatu nao walikaa nyegezi na shirika likawa limesimama. Mnamo mwaka 1989 Hayati Askofu Mkuu Antony Mayala alipochaguliwa kuwa Askofu wa Mwanza alifanya mpango wa kulihuisha upya tena shirika hili la Mabradha wa Moyo mtakatifu wa Yesu likiwa na mabradha wawili ambao walikuwa wamebakia.Hayati Askofu Mkuu mayala aliomba mabradha wa shirika la Banakaroli kutoka jimbo la masaka nchini Uganda kuja kusaidia malezi kwa shirika hili , Mpango huo ulilete mawazo chanya yaliyoweza kuzaa matunda baada ya mkuu wa shirika hilo kukubali ombi la askofu mayala na kuja kuanza kutekaleza kazi hiyo mara. Banakaroli walianza kulea vijana wale walioingia kwenye malezi ya kuwa mabradha, na june 1993 wanovis waliweka nadhiri za kwanza na shirika likaendelea na wanashirika walipokuwa wengi Banakaroli walirudi shirikani kwao na wanashirika wazarendo wakashika hatamu.
Shirika la moyo mtakatifu mpaka sasa linajumla ya mabradha 16, baadhi yao wanafanya utume maparokiani, nyumba ya askofu, taasisi na wengine wako shule na vyuoni. Shirika hili bado liko na mahangaiko kwani halijajiimalisha kusimama vizuri katika Nyanja zote kwa ujumla.Shirika la Moyo Mtakatifu wa yesu Nyumba yake mama iko MWAHOBA,Ndani ya parokia ya Nh'ungumalwa Jimbo la Mwanza.
Utume wa shirika
Kueneza injili katika jimbo kuu la Mwanza kwa kufanya huduma za kichungaji parokiani na kupokea utumishi mbalimbali katika taasisi za jimbo kuu la Mwanza kadri wakubwa wa shirika wanavyoona inafaa. Pia ukarimu wa kizalendo.