Parokia Teule ya Mt. Ambrose wa Milani Nyang’hingi ni zao la Parokia ya Mt. Augustino Mkolani Jimbo kuu la Mwanza; Parokia inayohudumiwa na Mapadri wa shirika la Mt. Augustino. Shukrani kwa Mungu kwa kutujalia neema, baraka, afya na maarifa na hivyo Injili inaendelea kuhubiriwa na kuenea maeneo mbalimbali. Hali kadhalika mifumo mikuu ya kanisa katoliki inaendelea kuanzishwa maeneo mbalimbali. Shukrani kwa Mapadri, Watawa na watendaji walei waliohudumu na wanaohudumu Parokia ya Mkolani kwa mawazo na hatimaye jitihada za uwepo wa huduma za kanisa/kiimani katika eneo la Nyang’hingi. NYANG’HINGI KUWA JUMUIYA: Nyang’hingi ilikuwa jumuiya mwaka 1995 katika kigango cha Mkolani, Parokia ya Nyegezi, chini ya Paroko Peter Mwanjonde (apumzike kwa amani). Msimamizi wa jumuiya alikuwa Mt. Benedicto wa Afrika na idadi ya kaya zilizounda jumuiya ni takribani 25. Mipaka yake ilikuwa kuanzia Mkolani center yaani kituo cha daladala za kwenda mjini barabara ndogo inayopandisha mwelekeo wa mlimani, barabara ya lami mpaka darajani mwelekeo wa Buhongwa, hadi Nyasubi na mipaka ya Malimbe yaani kwenye majengo ya hostel ya Laurence Masha. a. Viongozi wa Jumuiya ya Mt. Benedicto Nyagh’hingi 1. Mwenyekiti – Mathias Bulima (kwa sasa anaishi Parokia ya Kitumba Jimbo Kuu la Mwanza) 2. Makamu Mwenyekiti – Mzee Kaparasio Kazimili (apumzike kwa amani) 3. Katibu – Isack Mabula John (anaishi Parokia ya Bulale) 4. Makamu Katibu – Anna Michael (apumzike kwa amani) 5. Mhazini – Peter Lupeja (apumzike kwa amani) 6. Kiongozi wa Sala – Paschal Samwel Shunashu (anaishi Parokia ya Mkolani) Baadaye Jumuiya ya Mt. Clara ilianzishwa baada ya Masista wa Mt. Clara kuhamia Nyang’hingi. Ilifuatiwa na Jumuiya ya Mt. Monica na hatimaye jumuiya zingine zilizopo mpaka siku ya uzinduzi. Hata hivyo kufikia muda wa uzinduzi, jumuiya zenye majina haya ya Watakatifu (yaani Mt. Clara na Mt. Monica) ziko Parokia ya Mkolani. b. Idadi ya waamini Wakatoliki Idadi ilikuwa takribani 106 NYANG’HINGI KUWA KANDA: Nyang’hingi ilitangazwa kanda mnamo mwaka 2010 chini ya usimamizi wa Watakatifu Malaika Wakuu. a. Ununuzi wa eneo na huduma ya misa Mnamo mwaka 2017 viongozi wa Kanda wakishirikiana na viongozi wa Halmashauri Walei Kigango cha Mkolani, chini ya usimamizi wa Baba Paroko, Padre Hilary Mushi (OSA), walinunua eneo kwa ndugu Charles Mwiibura kwa lengo la kujenga jengo la Kanisa la Kigango katika mtaa wa Nyang’hingi. Eneo liligharimu Tshs 18,000,000/= (milioni kumi na nane tu). Huduma ya misa ilikuwa inatolewa angalau mara moja kwa mwezi kulingana na ratiba za kichungaji za parokia na maombi ya waamini wa kanda. Misa zilikuwa zinafanyika katika eneo la kanda (kwenye matenti ya kukodi kwa ajili ya tukio) au katika familia za waamini. b. Mapadre waliohudumu: 1. Padre Edger Ngowi(OSA) , (Paroko wakati wa mwanzo wa Kanda) 2. Padre Benard Mlowe (OSA), (Paroko awamu ya pili) 3. Padre Hilary Mushi (OSA), (Paroko awamu ya tatu) 4. Padre Joel Nziku (OSA) 5. Padre Erastus Mgani (OSA) 6. Padre Athanas Nzengo (OSA) 7. Padre Efrem Festo Msigala (OSA) 8. Padre Xavery Masanja Kasase (OSA) 9. Na Mapadre wengine ndani na nje ya jimbo. c. Idadi ya waamini Wakatoliki Idadi ya waamini ilikuwa takribani 632 d. Uongozi wa Kanda: 1. Mwenyekiti – Sabines Masawe 2. Makamu Mwenyekiti – Erasto Mbilinyi 3. Katibu - Honest Kacharuzi 4. Makamu Katibu – Christina Chacha 5. Mhazini – Magreth Masawe akafuata Esther Rusendela NYANG’HINGI KUWA KIGANGO: Mwezi Mei, 2018 Baba Paroko, Padre Joel Melchior Nziku (OSA) aliipandisha hadhi kanda ya Watakatifu Malaika Wakuu – Nyang’hingi kuwa Kigango Teule na kupewa jina la “Kigango Teule cha Mt. Ambrose wa Milan – Nyang’hingi”. Kigango cha Nyang’hingi kilizinduliwa rasmi tarehe 01 Desemba, 2018 kwa adhimisho la misa takatifu. Kwa wakati huo kulikuwa na jengo la bati sehemu zote ambalo lilijengwa ndani ya siku za mwezi wa Novemba, 2018. Jengo hilo lilitumika kwa ajili ya huduma za misa na huduma zingine za kikanisa. Siku ya uzinduzi wa kigango pia ilifanyika harambee ya kukusanya pesa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo bora la kanisa. Jengo la bati lilibomolewa lote na kujengwa kwa awamu ya pili ili kupisha ujenzi wa kanisa bora. Lilijengwa katika siku za mwezi wa Machi, 2021 na kukamilika 18.03.2021. a. Kanda na Jumuiya zilizounda Kigango: Kigango kilikuwa kinaundwa na Kanda tatu (3) na jumla ya jumuiya 13 kama ifuatavyo:- Kanda ya Mt. Barnaba Mtume ilikuwa na jumuiya zifuatazo; 1. Jumuiya ya Mwenyeheri Kristina 2. Jumuiya ya Mt. Gabriel 3. Jumuiya ya Mt. Mathayo 4. Jumuiya ya Mt. Yohana Mbatizaji Kanda ya Mt. Joseph Mfanyakazi ilikuwa na jumuiya zifuatazo; 1. Jumuiya ya Mt. Andrea Mtume 2. Jumuiya ya Mt. Clara 3. Jumuiya ya Mt. Catherine wa Siena 4. Jumuiya ya Mt. Karoli Lwanga Kanda ya Mt. Yohana Paulo II ilikuwa na jumuiya zifuatazo; 1. Jumuiya ya Mt. Petro 2. Jumuiya ya Mt. Scolastica 3. Jumuiya ya Mt. Bernard 4. Jumuiya ya Mt. Benedicto 5. Jumuiya ya Mt. Sharbel Kuongezeka kwa jumuiya: Mwaka 2018, jumuiya moja (01) ya Mt. Ambrose wa Milan (Kanda ya Mt. Barnabas Mtume) iliundwa. Kigango cha Nyang’hingi kikawa na jumuiya 14. Kupungua kwa jumuiya: Mwaka 2021, Jumuiya tano (5) zilimegwa na kurudishwa Parokia ya Mkolani, yaani Jumuiya ya Mt. Andrea Mtume, Jumuiya ya Mt. Clara, Jumuiya ya Mt. Catherine wa Siena, Jumuiya ya Mt. Karoli Lwanga na Jumuiya ya Mt. Benedicto. Kigango kikabaki na kanda mbili (02) zenye jumla ya Jumuiya tisa (09) Kuongezeka kwa Jumuiya: Ulifanyika tena mgawanyo wa jumuiya na hivyo jumuiya mbili (02) zikaundwa kama ifuatavyo; 1. Jumuiya ya Mt. Rita wa Kashia (Kanda ya Mt. Yohana Paulo II) 2. Jumuiya ya Mt. Joseph Mfanyakazi (Kanda ya Mt. Yohana Paulo II) Na hivyo kufanya idadi ya jumuiya kuwa kumi na moja (11) ndani ya kanda mbili (02) b. Idadi ya waamini Wakatoliki Wakati Nyang’hingi inatangazwa kuwa Kigango idadi ya waamini Wakatoliki ilikuwa takribani 872 c. Mapadre na Masista waliohudumu: 1. Padre Joel Nziku (OSA), (Paroko wakati wa kanda) 2. Padre Serafin Mwageni (OSA), (Paroko aliyefuatia) 3. Padre Erastus Mgani (OSA) 4. Padre Cyril Mulupi (OSA) 5. Padre Efrem Festo Msigala(OSA) 6. Padre Motavika Gontado (OSA) 7. Padre Xavery Masanja Kasase (OSA) 8. Padre Edger Mlelwa (OSA) 9. Na Mapadre wengine ndani na nje ya jimbo 10. Sr. Plasidia Mashime (Shirika la Mt. Benedicto – Kawekamo) 11. Sr. Gloria Lile (Shirika la Mt. Benedicto – Kawekamo) d. Uongozi wa Halmashauri ya walei 1. Mwenyekiti – Sabines Masawe. 2. Makamu Mwenyekiti – Erasto Mbilinyi, Pareji Singira, Wilbert Bujiku. 3. Katibu - Honest Kacharuzi. 4. Makamu Katibu – Ananias Rutambuka, Esther Soko. 5. Mhazini – Esther Rusendela akifuatiwa na Noela Magoti. Makatekista waliohudumu Makatekista waliohudumu katika Kigango Teule cha Mt. Ambrose wa Milani – Nyang’hingi kwa mpangilio wao ni hawa wafuatao:- 1. Katekista Lucy James (alihudumu muda mfupi na kustaafu) 2. Katekista Andrew David Bushi (alihudumu baadaye akaenda masomoni) 3. Katekista Yohana Molla James (alihudumu hadi Aprili, 2024) 7. Vyama vya kitume vilivyokuwepo: 1. UWAKA 2. WAWATA 3. Karismatiki Katoliki 4. Utoto Mtakatifu wa Kipapa 5. Watumikiaji 6. Kwaya NYANG’HINGI KUWA PAROKIA TEULE: Nyang’hingi ilitangazwa rasmi kuwa Parokia Teule tarehe 23.01.2022 na kuwa tena si chini ya mamlaka ya Parokia ya Mkolani bali Parokia Teule inayojitegemea. Padri msimamizi/Paroko alitangazwa kuwa Dr. Gaudence N. Talemwa. Ni Padre wa Jimbo la Rulenge Ngara, akiwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustino (SAUT) – Mwanza. a. Kanda na Jumuiya zake: Kanda zilikuwa mbili na Jumuiya zilizounda Parokia teule zilikuwa kumi na moja (11). Kuongezeka kwa Jumuiya: Baadaye ulifanyika mgawanyo wa jumuiya na hivyo kuanzishwa jumuiya mbili (02) zifuatazo; 1. Jumuiya ya Mt. Fransisco wa Asizi 2. Jumuiya ya Mt. Elizabeth wa Hungaria Hivyo Jumuiya zikawa kumi na tatu (13). Kanda ya Mtakatifu Barnabas Mtume 1. Jumuiya ya Mwenyeheri Kristina 2. Jumuiya ya Mt. Gabriel 3. Jumuiya ya Mt. Mathayo 4. Jumuiya ya Mt. Yohana Mbatizaji 5. Jumuiya ya Mt. Ambrose wa Milan 6. Jumuiya ya Mt. Elizabeth wa Hungaria Kanda ya Mtakatifu Yohana Paulo II 1. Jumuiya ya Mt. Petro 2. Jumuiya ya Mt. Scolastica 3. Jumuiya ya Mt. Bernard 4. Jumuiya ya Mt. Sharbel 5. Jumuiya ya Mt. Rita wa Kashia 6. Jumuiya ya Mt. Joseph Mfanyakazi 7. Jumuiya ya Mt. Fransisco wa Asizi b. Ujenzi wa kanisa la kisasa Tarehe 13.04.2019 uchimbaji wa msingi wa Kanisa ulianza na baada ya wiki moja ujenzi wa nguzo kumi za awali ulianza. Ujenzi wa nguzo uliendelea kwa kadri rasilimali zilivyokuwa zinapatikana. Ujenzi uliendelea kwa hatua mbalimbali ikiwemo kukamilisha nguzo hadi hatua ilivyo siku hii ya uzinduzi. Hasa ni hatua ya kukamilisha ujenzi wa Sacristia, uezekaji, na hatua zingine. c. Idadi ya Waamini Wakatoliki Kwa mujibu wa takwimu za Juni, 2024 Idadi ya waamini Wakatoliki ilikuwa 1,430 d. Mapadre/ Mashemasi/Masista waliohudumu Parokia Teule 1. Pd. Gaudence N. Talemwa (Jimbo la Rulenge Ngara) 2. Pd. Deogratias Katai (Jimbo Kuu la Mwanza). Tarehe 23.06.2023 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya Igombe na hivyo hatimaye kuhama. 3. Pd. Eligius Leonidas (Jimbo la Kayanga na mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustino (SAUT) – Mwanza); ambaye amekuwa akimsaidia mara nyingi Paroko. 4. Na ma Padre wengine wengi ambao wamekuwa wakifika kutoa huduma, yaani wa ndani na nje ya Jimbo Kuu la Mwanza. 5. Shemasi na hatimaye Pd. Julius Sospeter. 6. Sr. Clare Justian (Shirika la Masista Mitume wa Upendo Upeo). 7. Sr. Octaviana Emilian (Shirika la Masista Mitume wa Upendo Upeo). 8. Sr. Advella Martine (Shirika la Masista Mitume wa Upendo Upeo). 9. Sr. Ida Longino (Shirika la Masista Mitume wa Upendo Upeo). 10. Sr. Cecilia Samson (Shirika Masisita wa Elizabet wa Hungaria). 11. Sr. Nathanaela Dotto (Shirika la Mt. Benedicto – Kawekamo). e. Viongozi Halmashauri ya Walei waliohudumu kwa mfuatano mpaka kufikia uzinduzi 1. Mwenyekiti – Sabines Masawe, Nesphory K. Subira 2. Makamu Mwenyekiti – Wilbert Bujiku, Laurent M. Sabini 3. Katibu - Honest Kacharuzi 4. Makamu Katibu – Esther Soko, Agnes Alberto 5. Mhazini – Noela Magoti, Wilbert Bujiku f. Makatekista 1. Katekista Yohana Molla James; aliyehudumu hadi April 2024 2. Katekista Christina Suzo Matupa; alianza kuhudumu Julai, 2024 g. Vyama vya kitume: 1. UWAKA 2. WAWATA 3. VIWAWA 4. Karismatiki Katoliki 5. Utoto Mtakatifu wa Kipapa 6. Watumikiaji 7. Kwaya 8. Moyo Mtakatifu wa YESU 9. Marian Workers 5. MAFANIKIO: NYANG’HINGI IKIWA PAROKIA TEULE Baadhi ya mafanikio ni kama ifuatavyo; 1. Kuendelea kutoa huduma za kiroho vema kwa kadri ya utaratibu wa kanisa Katoliki, hivyo dadi ya waamini inaendelea kuongezeka. 2. Kuendelea na ujenzi wa kanisa na kufikia hatua ya kuezeka na hatua zingine. Katika hatua zote za ujenzi mamlaka ya Parokia Teule haijawahi kukopa ila ni kutokana na majitoleo ya waamini na wadau wenye mapenzi mema toka nje ya Parokia Teule. Kukamilisha ujenzi wa Sacristia inayofaa ambayo ni sehemu ya jengo la kanisa linalojengwa. 3. Ununuzi wa nyumba ya Mapadri kwa msaada toka kwa Askofu Mkuu na Parokia za Jimbo Kuu la Mwanza. Asanteni sana kwa wote kwa kuisaidia Nyang’hingi kukamilisha lengo hilo. Thamani ya nyumba na kiwanja ni shilingi za kitanzania milioni mia moja na kumi tu (110,000,000/=). Mamlaka ya Parokia Teule Nyang’hingi ilinunua kwa ndugu Mathew Pembe Dunia (Mkazi wa Mwanza) 4. Kununua eneo na nyumba iliyokuwemo jirani na eneo la kanisa. Ukarabati wa nyumba hiyo ndogo ulifanyika na inatumika kuwa ofisi ya halmashauri ya walei. Thamani ya kiwanja na nyumba ni shilingi za kitanzania milioni thelathini na tano tu (35,000,000/=). Mamlaka ya Parokia Teule Nyang’hingi ilinunua kwa ndugu William Jonas Mashala (Mkazi wa Mwanza) 5. Idadi ya misa kuongezeka kutoka moja (01) hadi tatu (03). Maamuzi haya ni kutokana na idadi ya watoto kuongezeka hadi kufikia kiwango cha takribani kujaza kanisa wakati wa misa yao siku ya Jumapili (yaani misa ya 03) 6. Kufanikisha zoezi la kutembelea kila familia ya waamini Wakatoliki kwa matukio ya kubariki nyumba, kushirikishana mambo ya kiimani na kufanya sensa. 7. Kuongeza idadi ya jumuiya hadi kufikia kumi na tatu (13). 8. Kujitahidi kumudu michango ya kijimbo. 9. Kuendelea kuboresha mahusiano mazuri na wadau mbalimbali. 10. Kutengeneza Tovuti ya Parokia Teule. CHANGAMOTO Zifuatazo ni baadhi ya changamoto katika Parokia Teule ya Nyang’hingi; 1. kutokamilisha ujenzi wa miundombinu ya Kanisa mfano jengo la kanisa, ukumbi kwa ajili ya mafunzo ya kiimani (yaani Ubatizo, Komunio, Kipaimara, ndoa, n.k.) 2. Uchache wa jumuiya (yaani 13) kutokana na eneo la makazi kuwa dogo. 3. Mwitikio hafifu wa baadhi ya waamini katika matukio na majukumu ya kikanisa. MALENGO MAKUU YA BAADAYE 1. Kukamilisha ujenzi wa kanisa ili waamini wawe na sehemu inayofaa kuabudia na hivyo kukua kiimani na katika kuwajibika kwa maendeleo ya kanisa na taifa. 2. Kuzidi kuwaimarisha waamini kiimani na kwa elimu ya mambo mengine ya kidunia kupitia majumuiko ya ibada na semina mbalimbali. Lengo ni kuwafanya wawe na ufahamu wa mambo, ujuzi, uzoefu na maarifa. Imani yetu ni kuwawezesha kukuza kipato ili kumudu maisha yao binafsi na kuweza kuwa wachangiaji wazuri wa shughuli za maendeleo ya kanisa na za kijamii. 3. Kununua viwanja zaidi kwa nia ya kufanya uwekezaji; kama vile, a. Kujenga shule. b. Kuwa na karakana za ufundi mbalimbali. c. Kujenga nyumba za kupangisha. d. Kujenga kumbi/ vyumba kwa ajili ya matukio mbalimbali. 4. Kununua vifaa vinavyoweza kukodiwa katika sherehe na matukio mbalimbali. 5. Kusaidia wahitaji katika namna mbalimbali pia kusomesha wadau mbalimbali kwa nia ya kuwa wakifanikiwa wanaweza kutoa fadhila kwa Parokia yetu au kuwa sehemu ya watendaji wanaofaa katika Parokia za Jimbo Kuu la Mwanza na katika jamii. 6. Kuendelea kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali. SHUKRANI Shukrani sana kwa Baba Askofu Mkuu Mhashamu Renatus Leonard Nkwande kwa kukipandisha hadhi Kigango cha Nyang’hingi kuwa Parokia Teule na hatimaye kuamua izinduliwe tarehe 31.08.2024. Shukrani pia kwa mamlaka zote za Jimbo Kuu la Mwanza kwa ushirikiano na ushauri. Shukrani kwa Mapadri, Watawa, waamini na wadau wote waliosaidia Patokia Teule ya Nyang’hingi kwa huduma, michango ya hali na mali kufanikisha maandalizi na hatimaye uzinduzi. UZINDUZI PAROKIA YA NYANG’HINGI; TUWE NA FURAHA NA TUISHI IMANI YETU.