Parokia ya Igombe
Parokia ya Mt. Mathayo Mtume na Mwinjili, ambayo awali iliitwa Parokia Teule ya Wat. Petro na Paulo Mitume Igombe, ikiwa ndani ya Parokia ya Mt. Yohana Mwinjili Nyang’wilolelwa, ikiwa na vigango vinne, ambavyo vilikuwa ni
1.Igombe.
2.Kabangaja.
3.Kilabela.
4.Kisundi, na Jumuiya kumi na tano(31).
Tarehe 27/12/2019 Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande aliipandisha hadhi Igombe na kuwa Parokia Teule chini Padre Yohana Shija Masalu aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Nyang’wilolelwa kwa wakati huo.
Tarehe 24/06/2023 Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande wa Jimbo Kuu la Mwanza aliisimika rasmi Parokia Teule ya Igombe , kuwa Parokia Kamili na kuitwa Parokia ya Mt. Mathayo Mtume na Mwinjili – Igombe. Akimtaja na kumsika Paroko wake wa Kwanza Padre Deogratias Katai. Na kuifanya kuwa Parokia yenye vigango sita ambavyo ni:-
1. Kigango cha Igombe.
2. Kigango cha Kabangaja.
3. Kigango cha Kayenzendogo.
4. Kigango cha Kilabela.
5. Kigango cha Kisundi.
6. Kigango cha Kasang’wa.
Vigango hivi vikiwa na Jumla ya Jumuiya ndogondogo za Kikristu 36 na Idadi ya Waumini wabatizwa wapatao 600. Parokia ikiwa kwenye udekano wa Kirumba nyakati hizo na kwa sasa ni udekano wa Ilemela. Parokia hii Kijiografia Kusini inapakana na Parokia teule ya Isanzu, Kaskazini Ziwa Victoria, Mashariki Parokia ya Kayenze na Magharibi Parokia ya Nyang’wilolelwa.
Parokia inauongozi uliokamilika pamoja na vyama vyote vya kitume.
Parokia inaendelea na mchakato wa kumaliza ujenzi wa kanisa la parokia, na ujenzi wa kanisa kwa vigango ambavyo ni vipya.
Ambavyo ni Kisundi, Kilabela na Kasang’wa.