Parokia yetu ya Mt. Josephina Bakhita ilianzishwa mwaka 2003 ikijulikana kama Kigango cha Mt. Josephina Bakhita kikiwa na jengo la kanisa lililojengwa kwa mabati kuanzia chini mpaka juu. Mwaka 2005 tulianzisha ujenzi wa Kanisa kubwa la kisasa ambapo ujenzi wake badae ulisimama kwa muda wa miaka 16 kwani uliendelea tena mwaka 2021 chini ya Baba Paroko Fabiani Ngeleja na mwaka huu tutamalizia boma  lake.

Mwaka 2011, Tulijenga Kanisa ambalo tunasali sasa na tukahama kutoka Kanisa la mabati tukiongozwa na Paroko Fransis Mtema Paroko wa Kirumba kwa sasa.

Mwaka 2016, Mhashamu Baba Askofu Mkuu Yuda Thadeusi Ruwaichi alitangaza kuwa Parokia teule. Baada ya kutanganzwa kuwa Parokia teule tulianza ujenzi wa nyumba ya mapadri na kukamilika.

Tarehe 19/09/2020, Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande alitangaza kuwa Parokia na kumteua Padre Fabiani Ngeleja kuwa Paroko wa Parokia ya Mt. Josephina Bakhita Nyamanoro. Ambapo leo 19/09/2024 Parokokia yetu imefika miaka minne kamili.

Baada ya kutangazwa kuwa Paroko, Baba Paroko Fabian Ngeleja aliripoti hapa Parokiani tarehe 1/10/2020 na kuanza utume katika Parokia yetu.

Tukumbuke kuwa, Parokia yetu ilitangazwa mnamo tarehe 19/09/2019 ikiwa na jumuiya 26 zenye mitaa minne(4) tu, ambapo kwa sasa Parokia yetu ina jumla ya mitaa kumi na moja (11) pamoja na jumuiya 38 na Kigango kimoja cha Mt. Thomas wa Akino Kilimahewa