Parokia ya Magu
Parokia hii kwa sasa inaongozwa na Paroko Pd. Onesmo Shingelwa ikiwa na takriban vigango 10. Pamoja na Paroko Pd. Onesmo Shingelwa Parokia imekua ikipata huduma kutoka kwa kwa Mapadre toka chuo cha SAUT na kutoka seminari ya Nyegezi. Parokia hii ilitoka katika Parokia ya Mt. Mt.Bernadetha Kahangara, ilizinduliwa rasmi mnamo mwaka 1978. Paroko wa kwanza alikua no Pd. John Soma mmisionari wa shirika la wamisionari wa Africa (White Fathers) akifuatiwa na Maparoko wengine takriban watatu wamisionari.
Padri wa kwanza mzalendo alikuwa ni Pd. Hilary Mfungo ambaye kwa sasa ni marehemu, baada hapo Parokia imehudumiwa na Maparoko takriban 12 akiwemo huyu wa sasa.
Ni Parokia iliyo mpakani na Jimbo la Shinyanga, Parokia hii iligawanywa na kupatikana Parokia nyingine ya Ihimbili.
Miradi
Parokia imeweza kujenga vibanda vya biashara vipatavyo 50 ambavyo vinachangia mapato ya Parokia lengo likiwa ni kuwapunguzia mzigo waumini na kuwa chanzo cha mapato ya Parokia. Pia wapo katika ujenzi wa kanisa kubwa ili kuendana na idadi ya waumini inayo ongezeka.
Kati ya waliowahi kuhudumu katika Parokoa hii ni Pamoja na Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande wa Jimbo Kuu la Mwanza akiwa Shemasi.