Kigango cha Mahina kilianzishwa na Wamisionari wajerumani mnamo mwaka 1891. Walimleta Stephano Mlingwa Busomile mwaka 1945 akiwa ni Katekista wa tano wa kigango hiki kutoka Kada Bujashi na Kumkabidhi Ardhi yenye ukubwa wa Ekari kumi na Tano (15) kwa ajiri ya shughuli za kanisa.
Mwaka 1989 Kigango hiki kilikabidhiwa katika Parokia ya Nyakato chini ya Paroko William moron, Mmisionari wa Afrika kikiwa na Jumla ya familia tano ambazo zilikuwa zikisali katika kikanisa cha Mawe kilichojengwa na Wamisionari wa wakati huo.
Tarehe 14/06/1991 Baba Askofu Mkuu Anthony Petro Mayala aliweka jiwe la msingi kigango hiki na ujenzi wa kanisa ulianza chini ya Paroko Lini, Mmisionari wa parokia ya Nyakato na waumini waliongezeka na kusali kwenye kanisa hilo.
Mwaka 2007 Kigango cha Mahina kilizaa vigango vya Ihago ambacho kiko Parokia ya Mahina na Kigango cha Nyanguruguru ambacho kiko Parokia ya Mhandu.
Kwahiyo kwa kutambua umhimu wa kuwa na watenda kazi wengi shambani mwa Bwana Kigango kiliwasomesha wafatao kuwa Makatekista:- 1. Maria Hamisi (Ambaye kwa sasa ni mgonjwa)
2. Frola Misalaba (Anahudumu Ihago)
3. Zephania Kahema ( yuko Biharamro )
4. Joseph Kazungu ( Anahudumu Mahina )
Wenyeviti: Mwenyekiti wa kwanza na aliyesimamia ujenzi wa mwanzo wa kanisa ni Maria Hamisi, alifuatiwa na Ponsiani Fumbuka, ndiye aliyesimamia uanzishwaji wa Vigango vya Ihago na Nyanguruguru, Lukas Masama alipigania sana ulejeshwaji wa eneo la Kanisa kwani baada ya Kifo cha Katekista Stephano kulijitokeza uuzwaji holela wa eneo la Kanisa na kwa sasa limebaki Ekari nne tu. Ndugu Crement Michael alishikilia uenyekiti wa mda mfupi lakini aliacha sifa nzuri za utunzaji wa kumbukumbu za Kanisa na hatimaye Bitrice Muta alichaguliwa mwaka 2013 na amedumu madarakani kwa miaka sita hadi leo tunapozindua Parokia hii.
Mwaka 2014 Baba Askofu Mkuu Yuda Thadeus Ruwaichi alikipandisha Hadhi Kigango na kuwa sub-parish, Chini ya Paroko Anselem Somuda wa Parokia ya Nyakato.
Mwaka 2017 Baba Akofu Mkuu Yuda Thadeus Rwaich aliipandisha hadhi sub-parish ya Mahina na kuitangaza kuwa Parokia Teule. Chini ya uongozi wa Paroko wa Nyakato Fr. Nanah.
Tarehe 3/12/2018 Padre Canisius Milango Aliteuliwa na aliyekuwa Askofu mteule wa jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Askofu Renatus Leonard Nkwande kuwa Paroko wa Parokia Teule ya Mahina.
Ili kuendelea kuwa na hadhina ya nguvu kazi ya kanisa mwaka huu 2019 Parokia Teule imefaulu kumsomesha Ukatekista Daud Pondi.
Leo tarehe 28/10/2019 Parokia yetu inazinduliwa na kusimikwa rasmi na Baba Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Mwanza kwa kuikabidhi Parokia hii chini ya Maombezi na usimamizi wa watakatifu Simoni na Yuda ikiwa na kigango cha Ihago chenye jumuiya kumi na nane (18) na mitaa mitatu (4) Wakati kigango cha Mahina kikiwa na Jumuiya ishirini na tatu (23) na mitaa mine (4)
Watakatifu simoni na Yuda mtuombee