Parokia Teule ya Mwananchi ilianzishwa tarehe 4/4/1994 ikiwa na hadhi ya kigango kutoka Parokia ya Nyakato, ikiwa na Jumuiya tatu ambazo ni Mt. Veronica, Mt. Joseph Mfanyakazi na Mt. Cecilia. Ujenzi wa Kigango ulianza 2001 baada ya muumini mwenzetu kutoa kiwanja chake kitumiwe kwa matumizi ya kanisa. Kigango cha Mwananchi kilipandishwa hadhi na kuwa Parokia Teule tarehe 13/11/2016. Parokia ya Mwananchi iko ndani ya eneo la Kiserikali la mtaa wa Mwananchi na Susuni, ina jumla ya waumini wapatao 993 ambao wanaishi katika Jumuiya 14 ambazo ni:- Mt. Veronnica, Mt. Juliana, Mt. Martine, Mt. Yasinta, Mt. Basil Mkuu, Mt. Catherine, Mt. Polycarp, Mt. Philomena, Mt. Ladislaus, Mt. Elizabeth, Mt. Laurent, Watakatifu wote wa Mungu, Mt. MariaGoreth na Mt. Ambrose. Jumuiya hizi zimegawanyika katika kanda nne (4) Ambazo ni:- “A” yenye Jumuia za Mt. Veronica, Mt. Yasinta, Mt. MariaGoreth na Mt. Catherine. Kanda ya “Gabriel” yenye Jumuiya za Mt. Ladislaus, Mt. Elizabeth, Mt. Polycarp na Watakatifu wote wa Mungu. Kanda “C” yenye Jumuiya za Mt. Philomena, Mt. Ambrose na Mt. Laurent. Kanda “D” yenye Jumuiya za Mt. Martine, Mt. Juliana na Mt. Basil Mkuu. Parokia Teule ya Mwananchi inazinduliwa leo talehe 29/6/2021 na Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza. Watakatifu Petro na Paulo mitume - mtuombee