Idara ya Kichungaji

Historia na Maendeleo ya Idara ya Kichungaji

Idara ya Kichungaji Jimbo Kuu la Mwanza ni mojawapo ya idara zilizopo ndani ya Jimbo Kuu la Mwanza. Ilianzishwa mwaka 1989, yaani miaka 33 iliyopita, kama matokeo ya msisitizo wa Mtaguso wa Pili wa Vatican II (1962-1965). Mtaguso huu ulijadili hati 16, ikiwemo hati ya Gaudium et Spes, ambayo imejikita katika uchungaji wa kisasa.

Muundo na Utendaji wa Idara

Idara ya Kichungaji hutekeleza shughuli zake chini ya uongozi wa Mhashamu Baba Askofu Mkuu, na pia inaendeshwa na mkurugenzi wa idara na katibu mtendaji. Katika ngazi ya parokia, kuna Halmashauri ya Kichungaji inayoshughulikia masuala ya kichungaji chini ya uongozi wa Paroko.

Lengo la Idara ya Kichungaji

Lengo kuu la Idara ya Kichungaji ni kuunganisha waamini wa ngazi zote ili kuleta umoja kama familia ya Mungu. Hii inajumuisha kujali na kuwajibika kwa ajili ya wengine. Aidha, idara inajitahidi kupima na kutathmini shughuli za kichungaji kwa kufuata sera zilizowekwa ili kuhakikisha ufanisi na usalama wa shughuli hizi.