Parokia ya Kirumba

Parokia ya Kirumba ni miongoni mwa Parokia 12 zinazounda Udekano wa Kirumba, ikiwa na Parokia Teule 1 chini ya uongozi wa Dean, Padre Francis Mtema.


HUDUMA ZA KIPAROKIA

Hadi kufikia mwezi Desemba, mwaka 2024, Parokia ya Kirumba inahudumia Parokia Teule ya Ibanda pamoja na vigango 4 vya Kirumba, Mt. Lucia (Medical), Mihama, na Kigoto.

Katika kipindi hiki, Mapadre Canicius Milango na Boniphace Herman waliokuwa Wasaidizi wa Paroko walihama na Kwenda Parokia za Pasiansi na Mwabagole. Kutokana na huduma nyingi zinazotakiwa, Parokia ya Kirumba iliwapokea Mapadre Busanda na Mabheha kama Wasaidizi wa Baba Paroko ili kutoa huduma katika maeneo tofauti ya Parokia na kuwafikia waumini.


Huduma za Kichungaji

Katika Parokia, Huduma za Kichungaji hutolewa na Mapadre wakisaidiwa na Makatekista. Hata hivyo, idadi ya Mapadre waliopo Parokiani imekuwa haikidhi mahitaji ya Parokia. Kwa neema ya Mungu, Parokia imekuwa ikipata huduma za Kichungaji kutoka kwa Mapadre wanafunzi wa Vyuo mbali mbali katika Jimbo la Mwanza au kutoka kwa Mapadre wageni wa Parokia.

Huduma za Kichungaji:

  • Kuadhimisha Ibada Takatifu za Misa
  • Kuendesha ibada za mazishi
  • Kutoa huduma kwa wagonjwa
  • Kuwaandaa na kutoa Sakramenti mbali mbali kwa waamini
  • Kuendesha Semina na Katekesi ya neno la Mungu
  • Kuwafundisha watoto na vijana msimamo thabiti wa imani

Matukio ya Kiparokia na Kijimbo

Parokia pia ilihamasisha na kushiriki matukio mbali mbali ya Kiparokia na Kijimbo kama:

  • Ushemasi na Upadrisho
  • Jubileo za Mapadre na Parokia
  • Uzinduzi wa Parokia mpya
  • Harambee za Parokia Kijimbo
  • Ujenzi wa Cathedral

Ukarimu na Kutegemeza Jimbo

Parokia inajivunia kutoa msaada katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

  • Kusomesha Waseminari
  • Kutoa chakula cha Seminari
  • Kulisha nyumba ya Mapadre Wazee na nyumba ya Bb Askofu
  • Kuwasaidia wasiojiweza hata kama sio Wakatoliki

Huduma kutoka kwa Masista na Makatekista

Parokia inapata nafasi ya kuwafikia waumini wake kupitia kwa Masista 4 wa Shirika la Mabinti wa Kilimanjaro, ambao hufanya shughuli mbalimbali kama:

  • Kusimamia na kutunza fedha za Parokia
  • Kusimamia na kuendesha Chuo cha Ufundi
  • Kusimamia na kuendesha Shule ya Chekechea
  • Kuratibu na kufanya shughuli zote za Kanisani na Sakristia

Makatekista wanashughulika na:

  • Kuwatembelea Wagonjwa
  • Kufundisha dini mashuleni
  • Kufundisha Wakatekumeni, Watoto na Wakristo wanaotarajia kupokea Masakramenti
  • Kutoa msaada kwa changamoto na shida mbali mbali za waumini

Watumishi wa Parokia

Pamoja na Wahudumu wa Kichungaji, Parokia inao watumishi mbali mbali ambao wanasaidia katika kutimiza majukumu ya Parokia.


UIMARISHAJI WA MIITO MBALI MBALI

Parokia yetu inamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia neema ya kuendelea kuwalea vijana wenye nia na fursa ya kujitoa ili kumtumikia Mwenyezi Mungu. Parokia pia ina waumini waliojitambua na kujipatanisha na Mungu kupitia Sakramenti ya Kitubio.


Huduma za Kiroho

Parokia ya Kirumba iliwaalika Mapadri na Walei waliobobea katika masuala ya Katekesi, ambapo walifikia makundi mbali mbali ya Parokia ili kuamsha na kukoleza huduma za kiroho.

Vyama vya Kitume:

  • WAWATA
  • UWAKA
  • VIWAWA
  • Shirika la Utoto Mtakatifu
  • Moyo Mtatifu wa Yesu
  • Wafranciscani
  • Radio Maria
  • Mt. Augustino
  • Karismatiki
  • Neokatekumenato

Kwaya:

  • Mt. Anna
  • Bikira Maria Mama wa Msaada
  • Mt. Francisco Xavery
  • Mt. Theresia
  • Mt. Thomas
  • Mwenyeheri Anwarite
  • Mt. Maria Goreth
  • Mt. Mikaili Malaika Mkuu
  • Mt. Cesilia
  • Mt. Petro na Paulo
  • Shirikisho la Kwaya

Huduma za Kijamii

Kila mwaka, Parokia ya Kirumba inaendelea kutoa huduma za kijamii kama:

  • Kutoa michango ya fedha kwa wagonjwa na wahitaji
  • Kutoa misaada kwa wasiojiweza, ikiwa ni chakula, mavazi, karo, na mahitaji mengine

Huduma ya Ulinzi na Malezi ya Watoto

Kamati inayoshughulikia masuala ya watoto imeanzishwa ili kuwalinda na kuwalea watoto katika imani, kuepuka masahibu ya ulimwengu na kuwasaidia kukua kiroho.


Miradi ya Parokia

Ujenzi na Matengenezo ya Majengo ya Parokia

Parokia inapata mkopo kutoka Benki ya Mkombozi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na majengo ya Parokia Teule ya Ibanda, Vigango vya Kigoto, Mihama na Medical.

Miradi ya Kichungaji:

  1. Kituo cha Hija na Mafungo cha Familia Takatifu - Hii imekuwa ni nafasi ya uponyaji na uimarishaji wa Imani Katoliki.
  2. Chuo/Shule ya Muziki - Hutoa mafunzo ya muziki, ikiwemo ufundi wa kucheza kinanda na muziki wa kusoma na kuandika nota.

Mafanikio ya Mwaka 2024

Kwa mwaka 2024, Parokia imeshuhudia mafanikio yafuatayo:

  • Maandalizi ya kuzindua Parokia ya Ibanda ifikapo Julai 2025
  • Ongezeko la idadi ya Miito
  • Uendelezaji wa ujenzi wa majengo ya Kanisa
  • Miradi ya kukoleza imani