HISTORIA YA PAROKIA YA KRISTU MCHUNGAJI MWEMA – BUZURUGA
Kuanzishwa kwa Kigango na Parokia
Kigango cha Buzuruga kilizaliwa kutoka Parokia ya Nyakato tarehe 13/10/1992. Mnamo tarehe 26/10/2004, Mheshimiwa Baba Askofu Mkuu alitangaza rasmi Kigango cha Buzuruga kuwa Parokia Teule. Parokia hii ilizinduliwa rasmi kuwa Parokia kamili na Mheshimiwa Baba Askofu Mkuu Hayati Anthony Petro Mayala tarehe 26/11/2006, ikiwa na vigango vitatu: Nyasaka, Bugarika (Mwananchi) na Buzuruga.
Upatikanaji wa Eneo
Eneo la Parokia ya Buzuruga lilinunuliwa kutoka kwa Mzee Ally Jumanne mwaka 1992 kwa kiasi cha Tsh. 100,000 (Laki moja tu). Lina ukubwa wa hekta 2.5 na limepimwa rasmi na kutolewa hati miliki Plot No. 964 Kitalu HH Nyakato.
Viongozi Waanzilishi wa Parokia
Mapadre wa Kwanza:
Padre Antony Sami – CMF (2004 – 2006)
Viongozi wa Halmashauri ya Walei:
Innocent Walwa – Mwenyekiti
Justius Mwita – Makamu Mwenyekiti
John Chonja – Katibu
Cyriacus Lweyendeza – Katibu Msaidizi
Mercia Mondea – Mhasibu
Jiografia ya Parokia
Ukubwa wa eneo: Hekta 2.5, linalozungukwa na milima upande wa Kaskazini na barabara iendayo Nyambiti.
Idadi ya Jumuiya: 30
Idadi ya Mitaa/Kanda: 4 (A, B, C na D)
Parokia hii haina vigango, bali ina Kanda nne zinazoiunda.
Makadirio ya idadi ya waamini: 1,500
Vyama vya Kitume
Uwaka
Wawata
Viwawa
Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu
Vyama vya Karama
Watumikiaji
Moyo Mtakatifu wa Yesu
Rozari Hai
Radio Maria
Karesmatiki Katoliki
Kwaya ya Kristo Mchungaji Mwema
Kwaya ya Yohana Paulo wa II
Kamati za Idara katika Parokia
Kamati ya Kiuchungaji
Kamati ya Liturujia
Kamati ya Elimu
Kamati ya Mawasiliano
Kamati ya Sherehe
Kamati ya Ardhi na Mazingira
Kamati ya Familia
Kamati ya Karitas
Kamati ya Utume wa Walei
Kamati ya Afya
Kamati ya Katekesi
Kamati ya Ulinzi
Taasisi Zilizopo
Mnara wa Vodacom (sasa inamilikiwa na Tigo)
Orodha ya Maparoko Waliohudumu
Mwaka | Paroko | Paroko Msaidizi |
---|---|---|
2004 – 2006 | Fr. Anthony Sami | - |
2006 – 2010 | Fr. Jesuraj Michael | Kulandey Sami |
2009 | - | Fr. Stephen Arulsamy |
2010 | - | Fr. John Britto |
2010 – 2012 | Fr. Stephen Arulsamy | Fr. John Britto |
2012 | Fr. William Baskar | - |
2012 | Fr. Abel Mwarabu | Fr. John Britto, Fr. William Baskar |
2014 | Fr. Abel Mwarabu | Fr. Thadeus Mchomba, Fr. John Britto |
2016 | Fr. Abel Mwarabu | Fr. Jonas Chellappan |
2017 | Fr. Chukwuemeka Anyanwu | Fr. Jonas Chellappan |
2017 | Fr. Chukwuemeka Anyanwu | Fr. Emmanuel Vethamuthu, Fr. Gabriel Bolan |
2019 | Fr. Chukwuemeka Anyanwu | Fr. Midhun Pullickal |
2020 | Fr. Chukwuemeka Anyanwu | Fr. John Britto |
2021 | Fr. Chukwuemeka Anyanwu | Fr. John Britto, Rev. Bazilio Kyaligonza |
2022 (Julai) | Fr. Chukwuemeka Anyanwu | Fr. Bazilio Kyaligonza |
2022 (Oktoba) | Fr. Pius Nwankwo | Fr. Bazilio Kyaligonza |
2023 | Fr. Pius Nwankwo | Fr. John Obonyo |
2024 | Fr. Pius Nwankwo | Fr. John Obonyo |
Miradi ya Parokia
Ujenzi wa Kanisa (mpango wa upanuzi)
Ukumbi wa Matumizi Mbalimbali (tayari unatumika)
Vyanzo vya Mapato
Sadaka
Zaka
Harambee ya kila mwisho wa mwezi (maarufu kama Harambee ya Bluu)
Michango ya Jumuiya
Ukodishaji wa ukumbi
Wafadhili wa ndani ya Parokia
Huduma za Kiroho
Misa Takatifu
Sakramenti: Ubatizo, Komunio, Kipaimara, Kitubio, Ndoa
Kutembelea wagonjwa na kuwapa mpako wa wagonjwa
Mapadre wanatembelea waamini kwenye Jumuiya kwa ajili ya kuwaimarisha kiroho
Miito ya Kipadre
Mapadre waliotoka Parokia ya Buzuruga:
Felician Nuru
Steven Bikolwamungu
Waseminari: Watatu wanaendelea na wito wao
Idadi ya Makatekista: Wawili
Parokia Jirani
Kaskazini: Parokia ya Nyasaka
Mashariki: Parokia ya Nundu
Kusini: Parokia ya Mwananchi
Magharibi: Parokia ya Mabatini
Shughuli za Waamini
Wafanyakazi
Wafanyabiashara
Wajasiriamali
Wastaafu
Mafanikio
Ujenzi wa ukumbi
Ujenzi wa uzio kuzunguka Parokia
Ujenzi wa kanisa dogo la kuabudia
Ununuzi wa Generator kubwa
Mchango wa kila mwaka kwa Jimbo
Changamoto
Kuhama kwa waumini kutokana na uhaba wa viwanja
Mahudhurio hafifu kwenye vikao na Jumuiya
Changamoto ya barabara mbovu inayopunguza wateja wa ukumbi
Malengo ya Baadaye
Upanuzi wa Kanisa
Ujenzi wa Chekechea
Kuimarisha Elimu ya Dini Mashuleni
Shukurani
Tunawashukuru wachungaji wetu kwa kutuhudumia kiimani na kiroho. Pia tunawashukuru waamini wote wa Parokia ya Buzuruga kwa kuijenga Parokia yetu.
Orodha ya Jumuiya zinazounda Parokia ya Buzuruga
- Mt. Marko
- Mt. Batlomeo
- Mt. Yuda Thadei
- Mt. Dominicko
- Mt. Clement
- Mt. Mathayo
- Mt. Benedicto
- Mt. Secilia
- Mt. Thomas
- Mt. Magdalena
- Mt. Flora
- Maria Mama wa Mungu
- Bikira Maria Mlima Karmeli
- Mt. Martha
- Epifania
- Mt. Fransisco
- Mt. Don Bosco
- Mt. Raphael
- Mt. Pius X
- Mt. Ritha
- Mt. Alberto
- Maria Mama wa Yesu
- Mt. Gabriel
- Mt. Yosefu
- Mt. Paulo
- Mt. Michael
- Mt. Stephano
- Mt. Petro
- Mt. Yohana Mbatizaji
- Mt. Klareti