Parokia ya Nyamhongolo
Nyamhongolo ilianzishwa mwaka 1946 ikiwa chini ya Parokia ya Bugando. Kigango hiki kilijumuisha vijiji vya Busekwa, Nyamadoke, Kanyama, Ihushi, Ng’wakilu na Kahama. Mnamo mwaka 1953 Bujora ilipewa Parokia na kigango cha Nyamhongolo kikawa chini ya Parokia ya Bujora na wakati huo wote waamini walikuwa wakisalia kwenye majengo ya serikali (shuleni). Muumini mmoja aliyekuwa anaitwa Anastazia Nyamulaguwa alijitolea eneo na ndipo lilipojenga lilipo kanisa mama. Mwaka 2005 Igoma walipewa Parokia hivyo kigango cha Nyamhongolo kikatolewa Bujora kwenda Parokia ya Igoma. Mwaka 2017 kigango cha Mt. Michael kilitangazwa kuwa Parokia Teule ya Nyamhongolo kikijumuisha vigango vya Nyamadoke, Isela, Igogwe na Ilalila. Mnamo tarehe 27/02/2021 Parokia Teule ya Nyamhongolo ilizinduliwa rasmi kuwa Parokia na Padre George Nima Nzungu akasimikwa kama Paroko wa kwanza wa Parokia ya Nyamhongolo.
Mtakatifu Michael Malaika Mkuu mtuombee