Parokia ya Familia Takatifu Pasiansi
Parokia ya Familia Takatifu Pasiansi ilizinduliwa rasmi kama Parokia mwaka 2000. Kwa sasa inaongozwa na Paroko Fr. Alex Kitwala na Paroko Msaidizi Fr. Canisius Milango, ambao ni Mapadri wa Jimbo. Parokia hii ina mitaa saba na Jumuiya 35, zenye jumla ya familia za wakikristo wapatazo 420. Kijografia, Parokia ya Pasiansi inapakana na:
- Parokia ya Kawekamo (Magharibi)
- Parokia ya Bwiru (Kaskazini)
- Parokia ya Lumala (Mashariki)
- Parokia ya Kiloleli (Kusini)
Waseminari
Tunao waseminari wapatao saba (7) wa Seminari Kuu, wawili kati yao wakiwa ni Erick Kyaruzi na Denis Nkuba. Seminari ndogo ina vijana watano. Parokia pia ina watawa wa Shirika la Fransisko wa Mtakatifu Bernadeta kutoka Rulenge Ngara.
Wigo wa Taarifa
Shughuli za Kiparokia
Parokia imefanikiwa kutoa huduma mbalimbali za kiimani, ikiwemo:
- Wabatizwa: 339
- Komunio: 91
- Kipaimara: 101
- Ndoa: 19
- Misa za Marehemu: 12
- Mapadri hutembelea wagonjwa
- Ziara katika Jumuiya na Mitaa
Vyama vya Kitume
Parokia ina vyama mbalimbali vya kitume, vikiwemo:
- Uwaka
- Wawata
- Viwawa
- Utoto Mtakatifu
Maendeleo
- Ununuzi wa kiwanja
- Ujenzi wa nyumba ya Mapadri
- Kukodisha viti na uwakala wa benki na mitandao ya simu
Malengo ya Mkakati ya Miaka Mitano (2025 – 2029)
- Ujenzi wa nyumba ya Mapadri
- Kupanua Kanisa
- Kujenga goloto
- Kuweka Paving
- Kuendeleza kiwanja eneo la Lumala
- Kujenga vyumba vya maduka eneo la Kanisa
Malengo Madogo ya Mwaka 2024
Ununuzi wa eneo la Kigango
- Tumepata kiwanja katika eneo la Lumala kwa ajili ya kuanzisha kigango, ingawa taratibu za kisheria kwa kupata hati miliki bado zinaendelea kupitia mwanasheria wa Jimbo.
Ziara ya Baba Askofu Mkuu
- Tarehe 06/05/2024, tulifanikiwa kumpokea Baba Askofu Mkuu ambaye alitoa Sakramenti ya Kipaimara.
Ukuaji wa Kiroho
- Tumekuwa na maendeleo makubwa ya kiroho na kiimani katika Parokia yetu kupitia Jumuiya zetu mbalimbali, vyama vya kitume, na shughuli za semina. Tunawashukuru Mapadri wetu, Fr. Alex Kitwala na Fr. Canisius Milango, kwa mchango wao mkubwa katika kukuza imani yetu.
Kuhudhuria na Kuchangia Matukio ya Kijimbo
- Parokia yetu imekuwa ikishiriki katika matukio mbalimbali ya Kijimbo, ikiwa ni pamoja na Ushemasi, Upadrisho, uzinduzi wa Parokia, na harambee za kijimbo. Tumekuwa pia tukichangia michango inayoagizwa na Jimbo na TEC.
Malengo Yaliyofanikiwa
- Ujenzi wa nyumba ya Mapadri – Endelea hadi sasa.
Malengo Yaliyoshindikana
- Kupanua Kanisa
- Kujenga goloto
- Kuweka Paving
- Kujenga vyumba vya maduka eneo la Kanisa
Malengo Madogo ya Mwaka/Kipindi Kinachofuata
- Kuendeleza kiwanja cha Kigango eneo la Lumala.
- Kuandaa harambee itakayowezesha kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Mapadri na kulipa madeni yaliyopo.
- Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Kijimbo, vikao, semina, na matukio mbalimbali.
- Kushirikisha waumini, hasa ngazi ya Jumuiya, kutekeleza shughuli za kijimbo kwa wakati husika.
- Kuimarisha Imani ya Kanisa Katoliki kwa Wanaparokia.
Changamoto
Baba Askofu Mkuu, tunakutana na changamoto kadhaa, hasa upande wa kiimani. Waumini wetu bado wanahitaji elimu zaidi ya Katekesi, na suala la ushiriki wa michango ya kikanisa, kama Zaka, Sadaka, na michango ya Utume wa Walei, linahitaji maboresho.
Hitimisho
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutekeleza mengi kwa mwaka 2024, licha ya changamoto mbalimbali. Tunaendelea kuwashukuru viongozi wa Jimbo kwa miongozo yao ambayo inatufanya tuendelee kutembea kisinodi.