Historia ya Parokia ya Buswelu: Tangu Mwaka 1918 Hadi Parokia Kamili Mwaka 2018

1. Misingi ya Parokia ya Buswelu

Kigango cha Buswelu kilianzishwa mwaka 1918, kikiwa chini ya Parokia ya Bugando, na uongozi wa Kat. Sililo Buhuta Mayanga na William Magolanga. Wakati huo, waumini walikuwa wakisali Kilatini tu, na eneo la kwanza kusali likawa Buswelu "B" kwao na Father Fabian Mayunga, chini ya mti uitwao "Nkobe" katika Jamii ya Mkuyu.

2. Mabadiliko na Uongozi wa Parokia

Baada ya muda, Sililo Buhuta Mayanga alihamishiwa Kagunguli Ukerewe, na kigango kilibaki chini ya uongozi wa William Magolanga. Enzi hizo, waumini walikuwa wachache, lakini walijumuika na waumini kutoka Sumba na Kahama.

Katika kipindi cha miaka ijayo, wakristo wa Buswelu walijenga kanisa la mawe huko Sumba na baadaye walihamia kwa William Magolanga kwa sababu ya umbali mkubwa.

3. Kuanzishwa kwa Parokia ya Bujora

Mnamo mwaka 1954, Parokia ya Bujora ilianzishwa, na kigango cha Buswelu kilihamishiwa kutoka Bugando. Uongozi wa Parokia ulipitia mabadiliko kadhaa, na baada ya kifo cha William Magolanga mnamo mwaka 1963, Bazil William alichukua jukumu la kuongoza kama Katikista.

4. Ujenzi wa Kanisa

Mwaka 1965, Nicodemus Ng'hanya alitoa eneo lake kwa ajili ya kujenga kigango cha muda, kilichojulikana kama Kigango cha Mt. Petro Bulola. Huu ulikuwa mwanzo wa juhudi za kujenga kanisa la kudumu.

Ujenzi wa kanisa ulianza mwaka 1974. Hata hivyo, juhudi hizo hazikufanikiwa kutokana na mvua zilizoharibu michoro ya ujenzi.

5. Kuendelea na Ujenzi na Maendeleo ya Parokia

Mwaka 1984, waumini walijitolea kwa kujenga kanisa kwa nguvu zao, huku wakiendelea kutoa mchango na msaada.

Mwaka 1986, kanisa la awali lilifunguliwa na Paroko Thomas Namwaga alikiongoza.

Mnamo mwaka 2014, Askofu Mkuu Yuda Thadeus alitembelea Buswelu, na Parokia ya Buswelu ilikubaliwa kuwa Parokia Teule ya Mt. Thomas Mtume.

6. Uhamisho na Hadhi ya Parokia

Tarehe 01/01/2018, Parokia Teule ya Mt. Thomas Mtume ilipandishwa hadhi na kuwa Parokia kamili, na Paroko wa kwanza alikuwah Pdr. Francis Kangwa (Marehemu).

7. Mapadri Waongozi wa Parokia

Parokia ya Buswelu imepata kuhudumiwa na Mapadri wafuatao:

  • Pdr. Francis Kangwa
  • Pdr. Gilbert Bujiriri
  • Pdr. Victa Sanou
  • Pdr. Jonson Singarajan
  • Pdr. James Meche Ryoba

Kwa sasa, Parokia inaongozwa na Pdr. Louis Ntamati na Paroko msaidizi Pdr. Joseph Chipimo.

8. Vyama vya Kitume na Kamati za Parokia

Vyama vya kitume vilivyopo parokiani ni pamoja na:

  • WAWATA
  • UWAKA
  • VIWAWA
  • UTOTO MTAKATIFU
  • WATUMIKIAJI
  • MOYO MT.
  • WAZEE WASTAAFU
  • KAMATI YA HIJA
  • KARISMATIKI KATOLIKI
  • KWAYA

Kamati za Parokia ni:

  • Kamati ya Malezi na Familia
  • Kamati ya Elimu na Mafundisho ya Dini
  • Kamati ya Ulinzi, Haki na Amani
  • Kamati ya Litrujia
  • Kamati ya Kichungaji

9. Geografia ya Parokia

Parokia ya Buswelu inapakana na parokia teule ya Nyamadoke upande wa Mashariki, na parokia ya Nyakato upande wa Kusini. Upande wa Magharibi inapakana na Parokia ya Kangaye na Nsumba, na upande wa Kaskazini inapakana na Parokia ya Kahama.

Parokia ina vigango vine vyenye jumla ya Jumuiya 67.

10. Jumuiya za Kigango cha Buswelu

Kigango cha Buswelu lina jumuiya 46, zikiwemo:

  • Bikira Maria Afya ya Wagonjwa
  • Mt. Gaspar Del Bufalo
  • Mt. Elizabeth
  • Mt. Gabriel
  • Yesu wa Msalaba
  • Mt. Kizito
  • Mt. Monica
  • WAT Cosma na Damiano
  • Mt. Veronica
  • Mt. Stephano
  • Mt. Yohane Paul II
  • Mt. Coletha
  • Mt. Augustino
  • Mt. Ambrose wa Milano
  • Mt. Gregory Mkuu
  • Mt. Francis wa Asizi
  • Mt. Francis Ksaveri
  • Mt. Benedicto
  • Mt. KaLoli Luanga
  • Kristu Mfalme
  • Mt. Francisca wa Roma
  • Bikira Maria Mama wa Mungu
  • Mt. Maria Gorethi
  • Mt. Lucas
  • Mt. Ritha wa Kashia
  • Mt. Polycalp
  • Bikira Maria Mfungua Mafundo
  • Mt. Andrea
  • Mt. Yuda Thadei
  • Mt. Philomena
  • Mt. Anthony wa Padua
  • Mt. Raphael
  • Mt. Josephina Bakitha
  • Mt. Thomas
  • Mt. Mathayo
  • Mt. Petro
  • Mt. Asteria
  • Mt. Ayubu
  • Mt. Thresia Mtoto wa Yesu
  • Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili
  • Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni
  • Mt. Tharesia wa Avila
  • Mt. Magdalena wa Canosa
  • Mt. Brigita
  • Mt. Benard

11. Idadi ya Wakatoliki na Huduma za Misa

Idadi ya wakatoliki waliobatizwa inakadiriwa kuwa kati ya 6000 hadi 7000 waumini.

Huduma za misa: Kila siku, isipokuwa Jumamosi. Jumapili kuna misa tatu katika Parokia, na kila kigango kinahudumiwa misa moja.

12. Changamoto na Malengo ya Parokia

Changamoto kubwa ni kutokuwa na imani thabiti kwa baadhi ya waumini, jambo linalopelekea wengine kuhamia kwenye madhehebu mengine.

Malengo makuu ni kumaliza ujenzi wa kanisa na gorotho la kuabudia, kuanzisha miradi ya Parokia kama shule na maduka, na kuimarisha waumini kiroho kupitia semina na mafundisho.

13. Shukrani

Tunatoa shukurani za dhati kwa Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande na wasaidizi wake kwa ushirikiano wao katika kuilea na kusimamia Parokia yetu. Pia tunatoa shukurani kwa Mapadri wa Shirika la Wamisionari wa Afrika kwa michango yao mikubwa katika huduma kwa waumini wa Parokia.