• archmwanza@gmail.com
  • +255 769 523 036

PAROKIA YA MT. MICHAEL MALAIKA MKUU - NYAMHONGOLO

Parish Details

HISTORIA  FUPI YA  PAROKIA  YA MT. MICHAEL MALAIKA MKUU -  NYAMHONGOLO  

 

Kigango cha Nyamhongolo kilianzishwa mwaka 1946 kikiwa chini ya Parokia ya Bugando. Kigango hiki kilijumuisha vijiji vya Busekwa, Nyamadoke, Kanyama, Ihushi, Ng’wakilu na Kahama. Mnamo mwaka 1953 Bujora ilipewa Parokia na kigango cha Nyamhongolo kikawa chini ya Parokia ya Bujora na wakati  huo wote waamini walikuwa wakisalia kwenye majengo ya serikali (shuleni). Muumini mmoja aliyekuwa anaitwa Anastazia Nyamulaguwa alijitolea eneo na ndipo lilipojenga lilipo kanisa mama. Mwaka 2005 Igoma walipewa Parokia hivyo kigango cha Nyamhongolo kikatolewa Bujora kwenda Parokia ya Igoma. Mwaka 2017 kigango cha Mt. Michael kilitangazwa kuwa Parokia Teule ya Nyamhongolo kikijumuisha vigango vya Nyamadoke, Isela, Igogwe na Ilalila. Mnamo tarehe 27/02/2021 Parokia Teule ya Nyamhongolo ilizinduliwa rasmi kuwa Parokia na Padre George Nima Nzungu akasimikwa kama Paroko wa kwanza wa Parokia ya Nyamhongolo.

 

Mtakatifu Michael  Malaika  Mkuu mtuombee

Parish Images

Parish Videos