Upadrisho Sahwa
Posted on: 01 Aug, 2024
Kuelekea adhimisho la Misa Takatifu ya Upadrisho katika Parokia ya Mt. Bathromeo - Sahwa
HISTORIA YA SHEMASI
NELSON MINZANI TIZOLEKEZA
A: KUZALIWA: Nelson
Minzani TIZOLEKEZA alizaliwa tarehe 20
April 1994 katika Kijiji cha Kashenge (Kilembo), Kata ya Katoma – Bukoba,
Kagera. Ni mtoto wa sita kati ya Watoto sita wa Baba Petro Paulo Rugaimukamu
(marehemu) na Mama Joanna Maria Kokubanza.
B: IMANI
KATOLIKI
UBATIZO: Alibatizwa Desemba 28, 1994 katika Parokia ya
Mtakatifu Yohane Mbatizaji- Katoma, Jimbo Katoliki la Bukoba. Namba ya Ubatizo
ni LB
4084.
KOMUNYO YA KWANZA: Desemba 28, 2000 katika Parokia ya
Mtakatifu Yohane Mbatizaji- Katoma, Jimbo Katoliki la Bukoba.
KIPAIMARA: June 11, 2006
katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji – Katoma, Jimbo Katoliki la
Bukoba.
C: ELIMU: Shule ya Msingi Katoma
“B” (2001-2008), 2009 -2012 Seminari ya Mtakatifu Maria – Rubya
Seminary iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba, Omumwani Sekondari na baadae Sekondari
ya Geita kidato cha V & VI (GESECO
2013-2015).
D: SAFARI YA
MALEZI YA WITO WA UPADRE:
Juni – Septemba 2015 Nyumba ya Malezi ya Mt. Yohane Paul II, Kawekamo – Jimbo
Kuu la Mwanza.
2015 – 2018: Masomo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Mt. Anthony wa
Padua, Ntungamo – Bukoba. 29 Novemba,
2015 alivikwa rasmi Kanzu, Ntungamo Seminari na Mha. Desderius Rwoma,
Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Bukoba.
2018-2023: Masomo ya Tauhidi (Teolojia) katika Seminari Kuu ya Mt.
Karoli Lwanga, Segerea – Dar es Salaam. 2019
alipewa Huduma ya Usomaji, Segerea Seminary- Dar es Salaam na Mwadhama
Kardinali Polycarp Pengo. 2020
alipewa huduma ya Utumishi Altare, Segerea Seminary- Dar es Salaam na Mha.
Renatus L. Nkwande, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza.
Julai – Novemba 2023:
Mwaka wa Kichungaji, Nyumba ya Baba Askofu Mkuu, Kawekamo.
Kuanzia Novemba 2023 hadi sasa, anaendelea na Masomo katika Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT-
MWANZA).
E: UTUME:
2016 – Parokia ya Buhingo.
2017 – Parokia ya Mt. Yustino - Bujora.
2018 – Parokia ya Mt. Francisko wa Asizi - Mbalika.
2019 – Parokia ya Kung’ara Sura kwa Bwana Wetu Yesu Kristo
- Mabatini.
2020 - Parokia ya Kung’ara Sura kwa Bwana Wetu Yesu Kristo
– Mabatini.
2021 – Parokia ya Mbalika na Nyumba ya Baba Askofu,
Kawekamo.
2022 – Nyumba ya Baba
Askofu, Kawekamo.
Daraja ya Ushemasi: Januari 06, 2024,
Kituo cha Hija Kageye (Parokia ya Kayenze) na Mha. Liberatus Sangu, Askofu wa Jimbo
Katoliki la Shinyanga.
Anawashukuru watu wote waliomsaidia katika safari ya masomo na malezi hadi kuifikia sikuu hii anapoijongea Altare ya Bwana. Anaomba tuungane naye na kusali pamoja naye leo anapotarajia kupewa Draja Takatifu ya Upadre ili Mungu amjalie uthabiti katika utume wake. Anaongozwa na maneno ya Nabii Isaya “Mimi hapa, Nitume mimi Bwana” (Isaya 6:8).
HISTORIA YA SHEMASI
GRAYSON WILBROAD
RUTAJUMBUKILWA
KUZALIWA:
Grayson Wilbroad
RUTAJUMBUKILWA alizaliwa March 15,
1991 Nyamagana-Mwanza (Tanzania). Ni mtoto Wa tatu kati ya watoto watano Wa
Baba Wilbroad William Rutahiwa na mama Hildagardas Protas.
IMANI KATOLIKI
Shemasi alibatizwa na kupata
komunio ya kwanza 25-12-2002 katika Parokianya Kristo Mfalme Nyantakubwa-jimbo
la Geita. Namba ya ubatizo ni 1984.
KIPAIMARA: June 20, 2004, parokia ya Yesu Kristo Mfalme
Nyantakubwa- Jimbo la Geita, na Mha. Askofu Damian Denis Daru. NB 10920.
ELIMU:
1998-2005: Shule ya msingi
2006-2007: Mwaka Wa malezi
Sayusayu -Shinyanga
2007-2010: Seminari ndogo ya
Makoko-Mara
2011-2013: high school Mwenge
-Singida
SAFARI YA MALEZI YA
WITO WA UPADRI:
2013-2014: Malezi ya
uasipiranti -nyumba ya malezi ya wamisionari Wa Konsolata-Morogoro
2014-2017: Masomo ya falisafa
-chuo kikuu Cha Jordan -Morogoro
2017-2018: Malezi ya unovisi-
Sagana -Kenya
07, 07, 2018: Nadhiri za
kwanza-Sagana Kenya. Na mkuu Wa shirika regione ya Kenya (Joseph Waithaka)
2018-2019: Malezi na mafunzo ya
Lugha (kiitaliano), mila na desturi- Roma-Italia
2019-2022: Masomo ya teolojia
(tauhidi)-Urbaniana
06,07, 2023: Nadhiri za Daima
na mkuu Wa shirika regione ya Ulaya (John Treglia)
08, 12, 2023: Daraja ya
ushemasi Jimbo kuu la Torino (Italia) na Mha. Askofu mkuu Roberto Repole.
2022-2024: masters katika
uchungaji (masters in Pastoral theology)-Chuo kikuu Cha
wasalesiani-Torino-Italia
UTUME:2013-Parokia ya
Nyantakubwa- Geita; 2014 parokia ya Mkundi -morogoro; 2014-2017-Parokia ya
Kasanga Morogoro; 2017-2018 kigango Cha Mitundu-Sagana (Kenya); 2018-2019:
parokia ya Mt Paulo Wa msalaba -Roma; 2020-2022: parokia ya Mt. Jerome-Roma;
2022-2024 Parokia ya Mt Joseph Kafaso-Torino+ utume kwa jumuia ya wahamiaji
kutoka Naijeria wanaoishi Torino (Italia).
Shemasi anatualika tusali
pamoja naye leo 08,08, 2024 anapotarajia kupewa daraja takatifu ya Upadri, ili
mungu amjalie kuwa imara katika kumtumikia, awe mwana wa Amani katika
kulihudumia Kanisa Kwa namna zote.(Yohane 14:27).
Tutto per un solo obiettivo “
la santità in Cristo Gesù
Everything good accomplished
for only one goal “holines in Christ Jesus “
Yote
Kwa lengo Moja ‘tu’ “Utakatifu katika Kristo Yesu”
Comments (0)
Post Your Comment