• archmwanza@gmail.com
  • +255 769 523 036

Historia Fupi Ya Parokia Ya Bulale

Parish Details

HISTORIA FUPI YA PAROKIA YA HURUMA YA MUNGU – BULALE

Parokia ya Huruma ya Mungu – Bulale ilianza mnamo mwaka 1980 kama kigango cha Mt. Maria, wakisali katika shule ya msingi Bulale. Mnamo mwaka 1990 Mzee John Linus (marehemu) alitoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa ili Waamini waache kusalia shuleni

Waamini walifurahi sana kwa kitendo hicho cha Mzee John Linus, hivyo walijenga Kanisa na kuliezeka kwa nyasi chini ya uongozi wa mzee John Linus (kama Mwenyekiti).

Baadaye wazee wa Bulale walipendekeza Msimamizi/somo wa kigango awe Mt. Isdori (Mkulima) kutokana na historia ya wakazi wa eneo hili kuwa wakulima.

Waamini waliendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kigango cha Mt. Isdori – Bulale kinapata maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuboresha jengo la Kanisa na kujenga choo cha kudumu.

Tarehe 6/07/2018 Kigango cha Mt. Isdori kilipandishwa hadhi kuwa Parokia Teule ya Bulale na Mhashamu Askofu Mkuu Yuda Thadaeus Ruwa’ichi na kuwekwa chini ya usimamizi wa Huruma ya Mungu ambapo leo tarehe 23/04/2022 inazinduliwa rasmi kuwa parokia kamili. Kanuni ya jumla ya utambuzi wa huduma za kichungaji huzingatia mipaka ya meneo, yaani ardhi (rejea CIC, Can 518). Kwa mantiki hiyo maeneo yanayotambulika kuwa ni Kigango mama cha Parokia Teule ya Huruma ya Mungu – Bulale.

Parokia hii teule ya Huruma ya Mungu Bulale, inajumuisha eneo lote la kanisa ambalo kwa sasa linafahamika kama Parokia teule ya Bulale, inayojumuisha vigango vya Bulale na Nyakagwe.

Kigango cha Bulale kina mitaa sita (06) yenye jumla ya jumuiya ishirini na tisa (29).

 

 

 

                                                

Kigango cha Nyakagwe kina mitaa mitatu (03) yenye jumla ya jumuiya kumi na tano (15).

Mhashamu Askofu Mkuu Renatus Nkwande aliikabidhi Parokia teule ya Huruma ya Mungu - Bulale chini ya usimamizi wa kichungaji wa Seminari ya Nyegezi ukiongozwa na Pd. Theophil Kumalija mwaka 2020 akisaidiwa na Pd. Bernadin Mtula, Pd. Sigismund Nyamungwa, Pd. John Nkwabi na Pd. William Ndonhe. Baadaye Pd. Kumalija alihamishwa na uongozi ukakabidhiwa kwa Pd. Mtula, pia aliongezeka Pd William Lebba na Shemasi Enock Mutegeki katika timu ya wachungaji.

Mpaka kufikia leo siku ya uzinduzi mambo kadhaa yamefanyika ikiwemo ujenzi wa nyumba ya mapadre (imekamilika), Choo cha Waamini cha kisasa na jukwaa la maadhimisho. Tunategemea pia kuanza ujenzi wa kanisa lenye hadhi ya parokia na kuweka uzio kuzungunka eneo la Parokia.

Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa baraka na maongozi yake kwetu wana Bulale; pia tunamshukuru Baba Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande kwa kuipandisha hadhi parokia hii teule kuwa parokia kamili.

Parish Images

Parish Videos