• archmwanza@gmail.com
  • +255 769 523 036

Parokia ya Mhandu

Parish Details

HISTORIA YA PAROKIA  YA  MHANDU

Kigango cha Mhandu kilianzishwa na Pd. William Moron aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Nyakato mwaka 1988. Kigango kilianza na jumla ya wakristo 20 ambao walikuwa wakisali kwenye chumba cha darasa katika shule ya msingi Mhandu.

Baadaye tarehe 22/03/1990 Paroko aliwanunulia eneo la ekali 7 kwa thamani ya Tsh. 82,000/= na wakaanza kujenga kanisa la matofali ya udongo mwaka 1994 na kuboresha eneo hilo kwa kupanda miti.

Tarehe 10/10/1994 walitangazwa kuwa kigango cha Mhandu kinachojitegemea chini ya Parokia ya Nyakato. Kigango kilianza na jumuiya 4 na vyama vya kitume viwili (2) Uwaka na Wawata.

Tarehe 02/08/2013 kigango kilipandishwa hadhi na kuwa Sub-Parish na Askofu mkuu jimbo kuu la Mwanza Jude Thadeus Rwaichi.

Tarehe 19/03/2016 Sub-Parish ya Mhandu iliteuliwa kuwa Parokia Teule na Askofu Mkuu Jude Thadeus Rwaichi.

Tarehe 28/11/2018 Pd. Vetrine Sumila aliripoti Mhandu kama Paroko Mteule wa Mhandu baada ya kuteuliwa na Baba Askofu mteule wa jimbo Kuu la Mwanza Renatus Nkwande.

Na leo 25/07/2019 Parokia yetu inasimikwa na kuzinduliwa rasmi na Askofu mkuu Renatus Nkwande, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza na kukabidhiwa kuwa chini ya maombezi na usimamizi wa Mt. Yakobo Mtume.

Parish Images

Parish Videos