• archmwanza@gmail.com
  • +255 769 523 036

HISTORIA FUPI YA PAROKIA YA SAHWA- MTAKATIFU BARTHOLOMEO

Parish Details

HISTORIA  FUPI YA  PAROKIA  YA MTAKATIFU BARTHOLOMEO - SAHWA

 

Parokia ya Mt Bartholomeo Sahwa ilianzishwa kama kigango mnamo mwaka 1994 na kuwa ni miongoni mwa vigango vilivyokuwa sehemu ya Parokia ya Nyegezi, chini ya Paroko Pd. Peter Mwanjonde na Katekista aliyehudumu wakati huo alikuwa ni Renatus Zephania  ambao kwa sasa  wote ni marehemu.

 

Mnamo mwaka 2007 baada ya Kigango cha Mt. Augustino Mkolani ambacho kilikuwa miongoni mwa vigango vya Parokia ya Nyegezi kupewa hadhi ya kuwa Parokia, Kigango cha Mt. Bartholomeo - Sahwa kiliwekwa chini ya Parokia ya Mkolani. Mwaka  2016  Parokia ya Mt. Monica Buhongwa ilizinduliwa, ambapo Kigango cha Mt. Bartholomeo Sahwa kilikuwa sehemu ya vigango vinne vilivyounda Parokia ya Mt. Monica Buhongwa, vigango vingine vilikuwa: Kigango Mama cha Mt. Monica Buhongwa, kigango cha Mt. Isdori Bulale ambayo kwa sasa ni Parokia ya Huruma ya Mungu Bulale na Kigango cha Mt. Yohane Chrisostom Lwanhima.

 

Mnamo tarehe 7 July mwaka 2018 Baba Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, wakati wa ziara yake ya kichungaji katika Parokia ya Mt. Monica Buhongwa, alitangaza kukipandisha hadhi kigango cha Mt. Bartholomeo Sahwa kuwa Parokia Teule chini ya  Parokia ya Mt. Monica Buhongwa, huku kikiwa chini ya usimamizi wa Baba Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa’ichi na Paroko Msaidizi akiwa Pd. Festo Ndiu – OSA.  Mwaka 2019 Parokia ya Buhongwa ilipata Paroko mpya Pd. Gontardo Fidelis Matavika - OSA, akisaidiwa na Pd. Athanas Edward Zengo - OSA, na baadae alifika Pd. Edgar Mlelwa - OSA kuwa Paroko Msaidizi, ambaye naye alihamishwa na kuja Padre Xavery Masanja OSA.  Mwaka huu mnamo mwezi June Parokia ya Mt. Monica na Parokia Teule ya Bartholomeo Sahwa tulipata Paroko mpya, Pd. Afrates Luambano - OSA, na Paroko Msaidizi Pd. Erasto Mgani – OSA ambao walitulea mpaka tuliposimikwa rasmi kuwa Parokia na kuwa chini ya Padre Joseph Ndalahwa kama Paroko wa kwanza wa Parokia ya Mt. Bartholomeo Sahwa.

 

Pia kwa namna ya pekee tunawashukuru mapadre mbalimbali waliotuhudumia kwa nyakati tofauti wakiwemo; Pd. Edgar Ngowi - OSA, Pd. Benard Mlowe – OSA, Pd. Joel Nziku - OSA, Pd. Ephraem Msigala - OSA, Pd. Cyril Mlupi - OSA, Pd.  Partrick Mpoli,  Pd. Ibrahimu Ngassa, Pd. George  Nima Nzungu, Pd. Akriatus Thobias, Pd. Bernadin Mtula, Pd. Basil.P.Rwezaura - OSB, Pd. Carlo J. Mwalongo, Pd. Deogratius Katai, Pd. Demitrius Njiku, Pd. John Makungu, Pd. Evarist Charahani, Pd. Fabian Ngeleja, Pd. Joseph Jamhuri, Pd. Engeibert Nyandwi, Pd. Paul Ngayomela, Pd. Seletine Nyanda na Pd. Moses Mapera na mapadre wengine kutoka Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT) Mwanza, Chuo Kikuu cha Sayansi Bugando (CUHAS), mapadre  wa shirika la Mt. Agustino na  jimbo kuu la Mwanza kwa namna moja au  nyingine ambao wamekuwa msaada kwetu wakati wote. Tunasema asanteni sana.

 

Tunamshukuru Mhashamu Baba Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi ambaye aliona hitaji na kutupatia hadhi ya Parokia Teule 07.07.2018. Mungu ambariki.

 

Aidha, kwa namna ya pekee tunakushukuru sana Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande kwa maongozi yako mbalimbali katika kulijenga Kanisa la Mungu, ambayo wakati wote yamekuwa ni dira na msaada mkubwa katika maendeleo ya Parokia hii hadi kufikia siku ya leo. Hakika sifa na utukufu ni kwa Mungu wetu Katika Kristo Yesu kwa ajili yako na Kanisa kwa ujumla kwetu.

 

Pia hatutawasahau makatekista waliowahi kuhudumu mahali hapa na wanao endelea, Katekista Renatus Zephania ambaye ni marehemu, Katekista Meshack E.Ndaki, Katekista Elias Katemani, Katekista Yohane Masinde, na makatekista wanao endelea kutuhudumia hadi sasa, Katekista Paskali Luchapa na Katekista Lidya Kokunyegeza.

 

Kigango kilipitia awamu mbalimbali za uongozi wa Halmashauri walei mpaka inakuwa Parokia Teule na kwa sasa viongozi wa Halmashauri walei ni hawa wafuatao:

 

Michael Daniel Masimbani………… Mwenyekiti

Rosemary Agustino Gesura………... Makamu mwenyekiti

Emmanuel Muhangwa Daud ……… Katibu

Nice Ernest Kanyabuhula………….. Katibu msaidizi

Rosada Paul Msaki………………… Mhazini

 

Asanteni kwa Huduma yenu na Mungu awabariki sana.

 

Parish Images

Parish Videos