• archmwanza@gmail.com
  • +255 769 523 036

Parokia ya Nyakahoja

Parish Details

Historia fupi ya Mtakatifu Fransisko Ksaveri.

Fransisko Ksaveri alizaliwa huko Uhispania, mahali palipoitwa Pamplona, mwaka 1506. Alitoka sehemu moja na Inyasi wa Loyola, lakini hawakuwahi kukutana hadi walipokuwa katika Chuo Kikuu cha Paris. Inyasi aliweza kumshawishi juu ya umuhimu wa kuyatoa kabisa maisha yao kwa Yesu Kristo na kwa ajili ya kazi yake. Ksaveri aliyekuwa mmoja wa Wajesuiti saba wa awali ambao waliyatoa kabisa Maisha yao kwa Bwana wetu huko Paris mahali palipojulikana kama Montmatre (maana yake kilima cha wafiadini) mwaka 1534.

Miaka saba baadaye, mwaka 1541, Ksaveri na washirika wengine wawili walitumwa na Inyasi kwenda kuyaeneza mafundisho na habari za maisha ya Yesu Kristo katika maeneo ya India yaliyokuwa chini ya utawala wa Wareno. Katika historia ya Ulaya, huu ulikuwa ndiyo wakati nchi nyingi zilikuwa zikitafuta masoko zaidi kwa ajili ya bidhaa zao pamoja na vyanzo vya kujipatia mali ghafi kwa ajili ya uzalishaji katika viwanda vyao.

Akiwa njiani kuelekea India, Ksaveri alisimama kwa muda mfupi hapa kwetu Afrika ya Mashariki, katika eneo la Malinda karibu na Mombasa. Baadhi ya askari wa Kireno waliokuwa wakisafiri naye waliaga dunia na akawazika hapa Malindi, ambapo pia alijenga kanisa dogo kwa ajili ya kumbukumbu yao. Hadi leo kanisa hili dogo bado lipo.

Kwa kipindi cha miaka saba, Ksaveri akifanya kazi miongoni mwa watu wa Goa, kusini kabisa mwa India, pia huko Sri Lanka, Malaysia, na Molucas, akiwa anarudi mara kwa mara kwenye makao yake makuu huko Goa. Mara nyingi Ksaveri aliwaandikia watawala wa Ureno kuhusu jinsi wavumbuzi wa Kireno walivyokuwa wakiwatendea vibaya wenyeji wa India. Kutokana na mafundisho yake watu wengi wa hali ya chini katika mfumo wa matabaka wa India walikuwa Wakristo.

Mwaka 1549 aliondoka Malacca kwenda Japani. Wakati huu alikuwa tayari amejifunza Kijapani kidogo. Pamoja naye walikuwa Wakristo watatu Wajapani. Alipofika huko, aliruhusiwa kufundisha na alipokelewa vizuri. Alikaa Japani kwa miaka miwili zaidi, hatimaye akaamua kuwa ilimbidi kusonga mbele kwenda China.


Miradi ya Parokia

Ili kuboresha na kurahisisha uendeshaji wa Parokia, kwa sasa Parokia ina miradi minne. Miradi hiyo ni Computer training Centre, Ukumbi, English & Kiswahili languages training centre pamoja na vyumba vya Ofisi.

Computer training centre

Kituo hiki hutoa mafunzo ya kompyuta kwa ufanisi mkubwa. Mafunzo hayo huwasaidia wale wanaojifunza kupata maarifa ya kurahisisha kazi zao kama kazi za kiofisi, za kiutafiti na kadhalika, kwa ubora na wepesi. Kituo kinapokea wote wanaopenda kujifunza na kuongeza maarifa yao ya matumizi ya kompyuta.

Ukumbi wa parokia

Ukumbi huu ni mradi muhimu sana katika parokia yetu. Parokia inatumia ukumbi huu uliojengwa kwa viwango vizuri kabisa katika baadhi ya mambo kama vile; sehemu ya kuendeshea semina na matukio mbalimbali ya kikanisa, kukodisha kwa watu kwa shughuli zao maalumu kama sherehe za harusi, vikao, uandishi wa mitihani, na mambo mengine yanayoendana na hayo.



Parish Images

Parish Videos