Parish Details
Parokia ya Sumve
Asili ya jina Sumve lilikuwa Busumabu lakini kutokana
na utata
wa matamshi kwa wazungu lilifupishwa mwanzoni na
kuwa
Sumva kisha likawa Sumve. Mapema mwaka 1897
makatekista
kutoka Bukumbi walitumwa Sumve, Nera, Ngasani na
Sumbuka,
ambapo vigango vikajengwa. Mapadre pale Rukumbi
wakawa
na shughuli nyingi kiasi kwamba wakashindwa
kuvitembealea
vigango hivyo mara kwa mara vikabaki chiral ya
uangalizi wa
makatekista.
Kuzinduliwa kwa uinjilishaji Rwanda kulisababisha
juhucli na
rasilimali watu vielekezwe zaidi huko. Miaka kumi ya
mwanzo
wa karne ya kumi na tisa hapakufanyika juhudi zozote
za
uinjilishaji kusini mwa Bukumbi. Pia Askofu Hirth
hakuona
umuhimu sana wa kuwekeza maeneo hayo. Mnao mwaka
1910
Padre Bourget na Huguenot walitumwa kutembelea Nera
na
Busumabu, wakakuta waprotestanti waliisha jitwalia
Nera.
Watawala wa Kikoloni hawakuruhusu mashirika mawili
ya dini
yenye ushindani kufanya shughuli zao sehemu moja.
Hivyo
Sumve
ikachaguliwa kwa unjilishaji mpya. Mwanzoni mapadre
waliishi katika pagale moja kubwa lililokuwa linatumika karna
darasa,
lilikuwa wazi bila milango wala madirisha. Usiku walilala
kwa hofu ya kuliwa na fisi au chui. Jitihada za ujenzi wa nyumba
zilianza kwa kuchoma
matofali i6o,000. Baada ya mwaka mmoja nyumba kubwa na nzuri ilikamilika.
Ikafuatia ujenzi wa Kikanisa cha ukubwa wa mt. 27
Mtemi Kibiti wa Usumao
akiwa na umri wa miaka 60, siku za nyuma aliishaalikwa na Askofu Hirth
kuhudhuria sherehe za kubariki kanisa la Bukumbi. Yeye alikuwa ni rafiki yake.
Hivyo mapadre hawakupata usumbufu. Walivutiwa na moyo wa juhudi na kazi
waliokuwa nao wasukuma katika kulima mtama ambao ulikabiliana na hali ya ukame,
na kilimo cha mpunga wakati wa masika na mazao ya mahindi, karanga na mhogo.
Walikuwa na utajiri wa mifugo, ng’ombe, mbuzi na kondoo. Mifugo yao hapo nyuma
ilishambuliwa na ugonjwa wa sotoka ikanusurika kutoweka. Walifika mara kwa mara
kwenye zahanati kwa ajili ya huduma za matibabu, lakini shuleni ni wazazi
wakristu ndiyo walioruhusu watoto wao kwenda shule licha ya juhudi kubwa na
ushawishi uliofanywa na mapadre kwa kuwatembelea majumbani mwao.
Walipinga hayo mafundisho
ya imani. Kijana mmoja wa miaka kumi na sita alikamilisha vizuri mafundisho ya
ukatekumeni. Kabla ya ubatizo baba yake alimtisha kuwa akibatizwa atakwenda
kuishi mbali na nyumbani kwao. Akaacha kuhudhuria Kanisani, lakini akaendelea
kusali nyumbani. Kupanuka na kuongezeka kwa ukristu Sumve kutafuatia na kuanza
kwa vita ya kwanza ya dunia.